Oct 14, 2021 07:33 UTC
  • Abdel Fattah al Sisi
    Abdel Fattah al Sisi

Mahakama ya kijeshi ya Misri imepasisha hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya watuhumiwa 32 waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za kuunda makundi ya kigaidi yaliyopanga njama ya kutaka kumuua Rais Abdel Fattah al Sisi wa nchi hiyo na mrithi wa zamani wa ufalme wa Saudi Arabia Muhammad bin Nayef.

Hukumu ya awali dhidi ya watuhumiwa hao ilitolewa mwaka 2019 na Mahakama ya Jinai ya Kijeshi katika kadhia iliyojulikana kama jaribio la kumuua al Sisi.

Wakili wa watuhumia hao amesema, Mahakama ya Juu ya Misri imekataa rufaa zote zilizowasilishwa na kupasisha hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya watuhumiwa 32 katika kesi hiyo.

Mwaka 2016 mwendesha mashtaka wa Misri alidai kuwa watu 290 wenye mfungamano na kundi la Kanda ya Sinai la kundi la Daesh walipanga njama ya kumuua Abdel Fattah al Sisi akiwa pamoja na mrithi wa zamani wa ufalme wa Saudi Arabia huko Makka mwaka 2014. Hata hivyo msemaji wa ikulu ya rais wa Misri wakati huo alikadhibisha madai ya kufanyika jaribio la kumuua al Sisi.  

Wanajeshi wa Misri katika jimbo la Sinai

Misri imekuwa ikikabiliiana na harakati za makundi ya waasi katika jimbo la Sinai kwa miaka kadhaa sasa na mwaka 2018 Cairo ilituma idadi kubwa ya wanajeshi kupambana na makundi hayo.

Tags