Oct 24, 2021 06:47 UTC
  • AIGP Asan Kasingye
    AIGP Asan Kasingye

Watu asiopungua watatu wanahofiwa kuaga dunia na karibu saba wamejeruhiwa vibaya katika mlipuko wa bomu uliotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo ya Komamboga Jijini Kampala kwenye eneo la kuuzia nguruwe, Tarafa ya Kawempe.

Watu walioshuhudia wameviambia vyombo vya habari kwamba wameona maiti za watu watatu baada ya mlipuko huo. 

Polisi ya Uganda walifika haraka eneo la tukio hilo na kulizingira mara moja na bado haitathibitisha kufariki dunia mtu yeyote katika tukio hilo.

Kamishna Mkuu wa Polisi, AIGP Asan Kasingye amesema kuwa, kulikuwepo mlipuko wa bomu na kwamba watu wawili wamejeruhiwa vibaya na wengine kadhaa wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mulago wakiwa na majeraha makubwa.

Vyombo vya usalama vya Uganda vinachunguza chanzo na sababu ya tukio hilo. 

Taarifa iliyotolewa na Polisi ya Uganda imesema: Timu za pamoja kutoka kikosi cha mabomu zinakagua eneo hilo ili kubaini iwapo mlipuko huo ulitokana na kitendo cha kukusudia au la. Polisi ya Uganda imewataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi wa kubaini kilichotukia ukiendelea. 

Tags