Oct 24, 2021 07:02 UTC
  • Ramtane Lamamra
    Ramtane Lamamra

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria ameikosoa nchi jirani ya Morocco kwa kuuingiza utawala wa Kizayuni wa Israel katika njama hatari dhidi ya serikali ya Algiers.

Ramtane Lamamra amesema kuwa, Morocco inaeneza habari za uongo kuhusu siasa za nje za Algeria na kwamba nchi hiyo imekua chanzo cha hali ya wasiwasi katika eneo la kaskazini mwa Afrika na kwamba inayatumia magenge ya kigaidi kwa ajili ya kuvuruga usalama wa nchi jirani.

Mwanadiplomasia huyo wa Algeria amesema kuwa, uvamizi wa morocoo huko Sahara Magharibi unalitumbukiza eneo hilo katika hali isiyojulikana. 

Tarehe 24 Agosti Algeria ilichukua hatua ya kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Morocco ikiituhumu Rabat kuwa imehusika na hatua kadhaa za kiuadui na kiuhasama dhidi yake. 

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria Ramtane Lamamra amesema uamuzi huo hauwezi kubadilika, umechukuliwa kwa kuzingatia maslahi ya taifa na kwamba, Algeria imekuwa na subira muda mrefu kabla ya kuchukua uamuzi huo ikivumilia chokochoko za jirani yake Morocco.

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, Morocco ilikubali kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel kwa sharti kwamba, Marekani iafiki mpango wa kuliunganisha eneo la Sahara Magharibi na ardhi ya nchi hiyo. Baada ya hapo rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump alitangaza kuwa Sahara Magharibi ni sehemu ya ardhi ya Morocco.

Hata hivyo kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Uadilifu ya Ulaya, hadi sasa nchi nyingi zimekataa kuitambua Sahara Magharibi kuwa ni sehemu ya ardhi ya Morocco.  

Tags