Oct 25, 2021 10:55 UTC
  • Kundi la Daesh latangaza kuhusika na mlipuko wa bomu Kampala, Uganda

Kundi la kigaidi la Daesh lenye itikadi za Kiwahabi limetangaza kuwa, wanachama wake ndio waliohusika na shambulio la mlipuko wa bomu katika mji mkuu wa Uganda Kampala siku ya Jumamosi.

Taarifa ya kundi la Daesh imeeleza kuwa, wanachama wake walilipua bomu katika eneo ambalo wanasema kuwa, majasusi wa serikali ya Uganda walikuwa wamekusanyika mjini Kampala.

Taarifa ya polisi Polisi ya Uganda imeeleza kuwa,  bomu hilo, liliulenga mgahawa unaouzwa nyama ya nguruwe katika viunga vya mji mkuu Kampala.

Uchunguzi uliokusanywa ulionyesha kuwa, wanaume watatu, waliojifanya kuwa wateja, waliweka mfuko wa plastiki chini ya meza na kuondoka muda mfupi kabla ya mripuko.

Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda  amelaani shambulio hilo la kigaidi na kusisitiza kwamba, vikosi vya usalama vya nchi hiyo litawasaka na kuwashughulia wale waliohusika na shambulio hilo la kigaidi.

 

Rais Museveni ameeleza bayana kuwa, "umma usihofu, tutazima uhalifu huu kama tulivyozima vitendo vingine vya aina hii, vilivyofanywa na nguruwe wasioheshimu maisha."

Watu wasiopungua watatu wanahofiwa kuaga dunia na karibu saba wamejeruhiwa vibaya katika mlipuko huo wa bomu uliotokea usiku wa kuamkia jana katika eneo ya Komamboga Jijini Kampala kwenye eneo la kuuzia nguruwe, Tarafa ya Kawempe.

Mwaka 2010 Uganda ilishambuliwa na magaidi wa Al Shabab wakati watu wakiangalia fainali ya kombe la dunia na kuua zaidi ya watu 70 kwenye uwanja wa raga wa Kyadondo na mgahawa wa Ethiopia Kabalagala.