Nov 12, 2021 02:23 UTC
  • Raia 15 wauawa katika shambulio la kigaidi nchini Nigeria

Watu wasiopungua 15 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiiwa katika viijiji vya kusini mashariki mwa Nigeria kufuatia mashambulio ya ulipizaji kisasi yaliyotokelezwa na kundi la majambazi.

Majambazi hao wakiwa na hasira ya kuuawa wenzao Jumatano iliyopita na raia wa maeneo hayo wameshambulia vijiji kadhaa kwa lengo la kulipiza kisasi na kuua kwa uchache watu 15 wasio na hatia.

Wakaazi wa maeneo hayo wameziambia duru za habari kwamba, hakuna afisa wa aina yeyote wa usalama aliyeko katika maeneo hayo na kwamba, hawana ulinzi wowote kutoka vyombo vya usalama kwa ajili ya kukabiliana na hujuma za majambazi hao.

Sambamba na matukio hayo, Nigeria inakabiliwa na hujuma na mashambulio ya kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo liimehatarisha maisha ya raia kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wanachama wa kundi la kigaiidi la Boko Haram

 

Tokea mwaka 2009 hadi sasa, Nigeria imo vitani kupambana na magaidi wa Boko Haram ambao wametangaza utiifu wao kwa genge la kigaidi la Daesh. 

Licha ya madai ya maafisa wa ngazi za juu katika jeshi la Nigeria kwamba, jeshi la nchi hiyo linaelekea kuwashinda wanamgambo wa Boko Haram lakini katika majuma ya hivi karibuni, wanamgambo hao wameshadidisha hujuma na mashambulio yao dhidi ya wanajeshi na raia. 

Hujuma na mashambulio ya  Boko Haram yameshaua watu wasiopungua 36,000 na kusababisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi ndani na nje ya Nigeria hasa katika maeneo yanayopakana na Ziwa Chad.

Tags