Nov 15, 2021 02:48 UTC
  • Moussa Faki Mahamat
    Moussa Faki Mahamat

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amesema umoja huo utatuma mjumbe nchini Sudan kwa ajili ya kutafuta suluhisho la mgogoro wa kisaisa nchini humo.

Moussa Faki Mahamat amesema kuwa, Umoja wa Afrika katika siku zijazo utatuma mjumbe nchini Sudan kwa ajili ya kuyakutanisha pamoja makundi yote ya kuyahamasisha kutafuta suluhisho la kisiasa la mgogoro wa nchi hiyo.

Mjumbe huyo atatumwa Sudan kwa mujibu wa wito uliotolewa na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

Moussa Faki Mahamat amesema kuwa, inasikitisha kuona kuwa, pande muhimu nchini Sudan hazijaafikiana kuhusiana na suala la kukabidhiana madaraka kwa njia za kidemokrasia na kukidhi matakwa ya wananchi. 

Vilevile amewataka watawala wa kijeshi wa Sudan kuanzisha mara moja mchakato wa kisiasa wa kurejesha utawala wa sheria na katiba. 

Wananchi wa Sudan wamekuwa wakifanya maandamano ya kila siku wakipinga mapinduzi ya kijeshi ya Jenerali Abdul-Fatah al-Burhan yaliyouondoa madarakani utawala wa mpito wa nchi hiyo.

Tags