Nov 21, 2021 08:12 UTC
  • Wanne wajeruhiwa Burkina Faso katika kupinga msafara wa kijeshi wa Ufaransa

Vyombo vya habari vimeripot kwamba raia wanne wa Burkina Faso wamejeruhiwa katika malalamiko ya kupinga kupita nchini humo msafara wa kijeshi wa Ufaransa kuelekea nchi jirani ya Niger.

Kwa mujibu wa vyombo hivyo, raia hao walijeruhiwa kwa risasi za onyo zilizofyatuliwa na wanajeshi wa Ufaransa walipokuwa katika msafara uliokuwa ukipita katika mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou kuelekea Niger, ambapo walikuwa miongoni mwa waaandamanaji waliojitokeza kupinga kupita msafara huo katika mji huo.

Kamandi kuu ya jeshi la Ufaransa hata hivyo imedai kuwa hakuna yoyote aliyejeruhiwa kwenye maandamano hayo lakini pamoja na hayo imekiri kwamba askari wa Ufaransa walilazimika kufyatua risasi ili kuwaogepesha watu iliodai walivunja ua la waya zinazozunguka kambi ambako wanajeshi wa Ufaransa walikuwa wamesimama kupumzika, kaskazini mwa mji mkuu wa Burkina Faso,Ouagadougou.

Kamaandi hiyo imesema msafara huo ulikuwa na malori 60 na askari 100.

Niger

Maandamano ya kupinga msafara huo yalianza siku ya Alkhamisi na yangali yanaendelea.

Niger ambayo ipo magharibi mwa Afrika licha ya kuwa na utahiri mkubwa wa maliasili ya mafuta na madinini ya urani lakini ni moja ya nchi masikini zaidi duniani.

Tukumbuke kuwa Mali na nchi hiyo jirani ya Niger ni maficho makuu ya shughuli za makundi ya kigaidi yakiwemo ya Daesh na Boko Haram. Machafuko na ukosefu wa usalama umeenea katika eneo hilo huku askari wa Ufaransa wakiwa wametumwa huko kwa miaka mingi sasa kwa kisingizio cha kulinda amani na usalama katika eneo hilo.

Tags