Nov 21, 2021 08:18 UTC
  • Maafa ya wahajiri kuelekea Ulaya; watu zaidi ya  75 wazama katika pwani ya Libya

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeripoti kuwa, wahamiaji haramu zaidi ya 75 wamefariki dunia baada ya boti yao kuzama katika pwani ya magharibi mwa Libya. Wahajiri hao haramu wamekumbwa na mauti Jumatano iliyopita katika jitihada za kuelekea barani Ulaya.

Shirika la IOM limeongeza kuwa, wahajiri hao haramu zaidi ya 75 walizama majini baada ya boti yao kuzama wakitokea Libya.  IOM imebainisha hayo kwa kuwanukuu wahajiri haramu walionusurika kifo ambao walifanikiwa kuokolewa na wavuvi na kupelekwa katika mji wa Zuwara. 

Hadi sasa wahajiri haramu zaidi ya 1,300 wamepoteza mwaka huu maisha kwa kuzama huko katikati mwa bahari ya Mediterania. Libya imetumbukia katiak hali ya machafukoge na ukosefu wa amani tangu kuangushwa utawala wa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011; na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa lango linalotumiwa na wahajiri haramu kuelekea barani Ulaya.

Kanali Muammar Gaddafi,  kiongozi wa Libya aliyeuawa baada ya kupinduliwa madarakani 

Wahajiri hao huku wakiwa katika boti za wanaojihusisha na magendo ya binadamu hujaribu kuelekea Ulaya wakitaraji kuwa  wakifika huko watakuwa na maisha bora kutokana na matatizo mbalimbali ya kiusalama na kiuchumi yanayozikabili nchi walikotoka. Wahajiri hao huhatarisha maisha yao kwa kufanya safari hizo katika bahari ya Atlantic au Mediterania kuelekea katika nchi za Ulaya. 

 

Tags