Nov 23, 2021 02:42 UTC
  • Waziri Mkuu wa mpito Libya naye pia ajitosa kwenye kinyang'anyiro cha urais

Siku moja kabla ya kufungwa kwa shughuli ya kuwasilisha fomu ya kuwania uchaguzi wa urais wnchini Libya, Waziri Mkuu wa mpito, Abdel Hamid Dbeibah, naye pia jana alijitangaza kuwa atawania katika uchaguzi huo.

Baada ya Seif al-Islam Gaddafii na Jenerali wa zamani wajeshi Khalifa Haftar, waziri mkuu wa serikali ya mpito Libya jana alitangaza kuwania kwenye kiti cha urais mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wakati hali inazidi kuwa ya wasiwasi, huku wengi wakiondoa matumani ya uchaguzi ho kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

Kulingana na sheria ya uchaguzi inayotumika nchini Libya, barua ya kuwania katika uchaguzi inaweza kukubaliwa tu ikiwa mgombea ataacha kazi rasmi anayoshikilia miezi mitatu kabla ya uchaguzi. Kaimu Waziri Mkuu aliye madarakani, Abdel Hamid Dbeibah hangeweza kwa mujibu wa sheria hii, kuwa mgombea.

Lakini kiongozi huyo wa serikali alipoteza imani ya wabunge Septemba 21, wakati wa kura katika makao makuu ya Bunge la Tobruk. Hata kama hajaacha wadhifa wake tangu wakati huo, Dbeibah anaendana na hoja hii ili kudai haki yake ya kuwa mgombea mbele ya sheria.

Kufikia sasa wagombe ambao wamesha tangaza kuwania katika uchaguzi huo ni watano, ikiwa ni pamoja na Khalifa Haftar kutoka Mashariki, Spika wa bunge Aguila Saleh, mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi, Seif al-Islam Gaddafi, Fatih Benchaga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kutoka magharibi mwa nchi na Abdel Hamid Dbeibah.../

 

Tags