Nov 25, 2021 04:42 UTC
  • Mapigano yashadidi Ethiopia, baadhi ya nchi zataka raia wake waondoke

Mapigano yanaripotiwa kushadidi nchini Ethiopia baina ya jeshi la serikali na makundi kadhaa ya waasi wanaongozwa na kundi la TPLF ambao wanaaminika kupata msaada wa kigeni.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema umoja huo umetangaza kuwahamisha wanafamilia wa wafanyakazi wake kutoka Ethiopia kutokana na ghasia,

"Kutokana na hali ya usalama nchini Ethiopia na tahadhari nyingi, Umoja wa Mataifa umeamua kupunguza uwepo wake nchini Ethiopia kwa kuwahamisha kwa muda wanafamilia wa wafanyakazi wake," Stephane Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema

Nchi kadhaa za Magharibi pia zimewataka raia wake  waondoke  Ethiopia mara moja, huku kukiwa na hofu kwamba vita vya ndani vya nchi hiyo vinakaribia kuongezeka.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Jumatatu ya wiki hii aliapa kuwa ataelekea mstari wa mbele kuwaongoza wanajeshi wake, na kutangaza: "Sasa tuko katika hatua za mwisho za kuiokoa Ethiopia."

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Maafisa wa serikali katika mji mkuu walisisitiza Jumanne kwamba vikosi vya usalama vinafanya kazi kuhakikisha amani na utulivu wa Addis Ababa unadumishwa na kuwaambia wanadiplomasia wasiwe na wasiwasi.

Eneo la Kaskazini mwa Ethiopia limekumbwa na uhasama tangu ghasia zizuke mwaka mmoja uliopita katika Jimbo la Tigray. Tangu wakati huo, vita vimeenea hadi Majimbo ya Afar na Amhara. 

Wakati huo huo siku ya Jumatatu, mjini Pretoria marais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na mwenzake wa Kenya  Uhuru Kenyatta walitoa wito kwa pande zote katika mpigano Ethiopia zisitishe uhasama