Dec 02, 2021 12:10 UTC
  • Kirusi kipya cha Omicron chagunduliwa Ghana na Nigeria

Ghana imetangaza kuwa wanasayansi wamegundua kesi kadhaa za aina mpya ya kirusi cha corona cha Omicron miongoni mwa wasafiri waliwasili nchini humo siku kumi zilizopita.

Patrick Aboagye Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Afya wa Ghana amesema kesi hizo mpya za Omicron zimetokea Nigeria na Afrika Kusini. 

Vipimo walivyochukuliwa kutoka kwa wasafiri waliowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kokota huko Ghana viligundua kuwa watu hao wameambukizwa kirusi kipya cha corona aina ya Omicron. 

Ripoti kutoka kwa William Ampofo mtaalamu wa virusi imethibitisha kuwa, vipimo vya wiki walivyochukuliwa kutoka kwa wasafiri 200 waliowasili katika uwanja huo wa ndege vimeonyesha kuwa, asilimia 28 ya watu wote waliowasili Ghana kutoka Nigeria na Afrika Kusini wamekutwa na maambukizi ya Omicron.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Ghana Francis Chisaka Kasolo ametilia mkazo umuhimu wa watu kupata chanjo ya kujikinga na UVIKO-19.  

Ghana na utoaji chanjo za corona 

Wakati huo huo Nigeria pia imetangaza kugundua kesi ya kwanza ya aina mpya ya kirusi cha corona kwa jina la Omicron kwa wasafri walioingia nchini humo wakitokea Afrika Kusini wiki iliyopita. Hayo yameelezwa na Taasisi ya Taifa ya Nigeria ya Afya ya Umma.