Dec 03, 2021 07:49 UTC
  • Mufti: Kuna njama zinazoungwa mkono na Wamagharibi za kuiangusha serikali ya Ethiopia

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ethiopia amesema kuwa, kuna njama ya siri inayopikwa ambayo lengo lake ni kuiangusha serikali halali ya nchi hiyo inayoongozwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

Akijibu swali kuhusiana na mkanda wa video ulioenea unaoonyesha baadhi ya wanadiplomasia wa Kimagharibi wakiwa katika mazungumzo na viiongozi wa Harakati ya Ukombozi ya watu wa Tigray (TPLF), balozi Dina Mufti amesema kuwa, mkanda huo wa video inaonyesha kuweko njama dhidi ya utawala halali wa serikali ya Abi Ahmed ulioingia madarakani kwa njia ya kidemokrasia.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ethiopia ameongeza kuwa, huu ni uingiliaji wa wazi katika masuala ya ndani ya nchi nyingine ambnao unakinzana wazi na hati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika pamoja na kanuni zinazotawala katika mahusiano baina ya mataifa mbalimbali, hivyo kitendo hicho kinapaswa kulaaniwa vikali.

Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia

 

Hivi karibuni serikali ya Ethiopia iliwatimua baadhi ya wanadiplomasia wa kigeni nchini humo, hatua ambayo imetathminiwa kama onyo dhidi ya uingiliaji wa masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Vita hivyo nchini Ethiopia vilianza Novemba 2020n baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kutoa amri ya kushambuliwa Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray TPLF baada ya kuwatuhumu wapiganaji wa harakati hiyo kuwa waliwashambia askari wa jeshi la serikali kuu.

Mapigano katika jimbo la Tigray yamepelekea maelfu ya watu kuuawa na wengine wengi kulazimika kuishi katika mazingira magumu ya kiafya na kukabiliwa na hatari ya baa la njaa.