Dec 04, 2021 07:46 UTC
  • Uchaguzi wa kwanza wa rais Gambia tokea Jammeh aondolewe

Wananchi wa Gambia wanapinga kura katika uchaguzi unaofanyika kwa mara ya kwanza tokea rais wa zamani Yahya Jammeh aondolewe madarakani.

Rais wa sasa Adama Barrow aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2016, amebainisha matumaini yake kuwa atashinda muhula wa pili katika uchaguzi wa rais unaofanyika leo Jumamosi.

Kwa ujumbla kuna wagombea sita wanaowania kiti cha urais katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Hata hivyo mchuano mkali unatabiriwa kuwa baina ya Rais Adama Barrow wa chama cha NPP na aliyekuwa Naibu wake Ousainou Darboe anayegombea kwa tiketi ya chama cha United Democratic Party (UDP).

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa mbili kwa saa za GMT na zoezi la upigaji kura linatazamiwa kuendele ahadi saa 11 GMT. Matokeo ya awali yanatazamiwa kutangazwa Jumapili.

Gambia ni kati ya nchi masikini zaidi duniani ambapo kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia, nusu ya wakazi wake milioni mbili wanaishi kwa pato la chini ya dola 1.9 kwa siku.

Wagombea wote wamesisitiza juu ya ajenda ya kuleta mabadiliko kwenye kampeni zao wakati ambapo raia wa Gambia wanaosaka haki nchini mwao,  wanataka uchumi imara baada ya taifa hilo pia kukumbwa na athari zilizosababishwa na janga la corona hali ambayo inachochea idadi kubwa ya watu wanaojaribu kuikimbia nchi hiyo kwa kutumia njia za hatari kwenda barani Ulaya.