Dec 04, 2021 11:24 UTC
  • Algeria: Morocco imetengwa kutokana na kuanzisha muungano wa kijeshi na Israel

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria amesisitiza kuwa, kadiri Morocco inavyochukua hatua yoyote ile ya kutaka kuimarisha muungano wake wa kijeshi haribifu na utawala vamizi wa Israel ndivyo inavyozidi kuwa mbali na Algeria.

Ramtane Lamamra ameeleza kuwa, muungano wa kijeshi baina ya Morocco na utawala wa Kizayuni unaotenda jinai dhidi ya Wapalestina ambao unalenga kuimarisha kujitanua pande  hizo mbili katika eneo la kaskazini mwa Afrika umefikiwa kwa gharama ya kuwatoa muhanga wananchi na kuwanyima haki zao za kimsingi.

Lamamra amesema kuwa, kwa mtazamo wa Algeria ni kuwa, mataifa ya Kiarabu badala ya kuusaidia utawala ghasibu wa Israel katika harakati zake za kujitanua katika maeneo ya Waarabu, zinapaswa kufanya juhudi za kuunga mkono haki za wananchi wa Palestina.

Msimamo huo wa Algeria unatangazwa masaa machache tu baada ya nchi hiyo kunukuliwa kupitia Waziri wake wa Mashauri ya Kigeni ikisisitiza kwamba, wananchi wa Algeria wataendelea kuwaunga mkono wananchi wa Palestina ambao nao kama walivyo watu wengine wana haki ya kujikomboa kunako ukoloni na uvamiz unaowakandamiza.

 

Algeria imekuwa mstari wa mbele katika miezi ya hivi karibuni kupinga sera na siasa za utawala ghasibu wa Israel na ukandaizahji wake dhidi ya wananchi wa Palestina.

Misimamo hiyo ya Algeria imeshuhudiwa zaidi hasa baada ya jirani yake Morocco kutia saini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na hivi karibuni kutia saini hatia ya kuanzisha ushirikiano wa kkijeshi na Tel-Aviv.

Tags