Dec 07, 2021 08:17 UTC
  • Jeshi la serikali ya Ethiopia lakomboa miji 3 ya kimkakati katika mapigano na waasi wa Tigray

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed asema kwamba vikosi vya nchi yake vimedhibiti tena udhibiti miji 3 ya kimkakati katika eneo la kaskazini la Amhara iliyokuwa mikononi mwa kundi la Tigray People's Liberation Front.

Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa vikosi vya serikali vimefanikiwa kuteka tena miji ya kimkakati ya Disi, Kombolcha na Bati na kwamba vimeimarisha udhibiti wa maeneo mengi ya mkoa wa Amhara na eneo lote la Afar. Amesema jeshi la taifa la Ethiopia limewatia hasara kubwa wanamgambo wa Tigray.

Abiy Ahmed ameongeza kuwa: "Maeneo yaliyovamiwa na wanamgambo wa Tigray  katika muda wa miezi mitano iliyopita, tumeyakomboa ndani ya siku 15."

Kundi la waasi wa Tigray lilikuwa limechukua udhibiti wa miji ya Disi na Kombolcha zaidi ya mwezi mmoja uliopita, na kutishia kusonga mbele kuelekea mji mkuu, Addis Ababa, jambo ambalo liliifanya serikali ya Ethiopia kutangaza hali ya hatari nchini kote.

Vikosi vya jeshi la serikali ya Ethiopia vimepata ushindi mtawalia tangu Waziri Mkuu wa nchi hiyo atangaze kwamba anasimamia mwenyewe mapigano ya nchi kavu dhidi ya waasi wa Tigray mwanzoni mwa Desemba.

Tags