Dec 09, 2021 04:39 UTC
  • Rais wa Niger akosoa udhaifu wa nchi jirani katika kupambana na ugaidi

Rais wa Niger amezikosoa nchi jirani katika mapambano ya kukabiliana na ugaidi na magendo ya silaha kutoka Libya katika eneo la Sahel Afrika.

Mohamed Bazoum ambaye alishika madaraka ya Niger yapata mwaka mmoja uliopita, anakabiliana na hali ya ukosefu wa usalama nchini humo na ukimbizi wa ndani ya nchi wa zaidi ya watu elfu 95 hususan katika eneo la Tillabéry.  

Niger pia imekumbwa na mashambulizi ya hapa na pale ya magenge ya kigaidi yenye uhusiano na makundi ya al Qaida, Daesh na Boko Haram.boko haram

Wapiganaji wa Bokko Haram

Rais wa Niger anaamini kuwa, hali hiyo ni matokeo ya makosa ya kistratijia na akiashiria udhaifu wa vyombo na asasi zenye jukumu la kupambana na magendo ya silaha kutoka Libya, nchi ambayyo ndiyo chanzo kikuu cha kudhamini silaha zinazotumiwa na makundi ya kigaidi huko Niger. 

Rais Mohamed Bazoum wa Niger amesema nchi za eneo la Sahel zinahitajia msaada na himaya ya washirika wake kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa usalama na ukatili unaofanywa na makundi ya kigaidi.  

Tags