Dec 15, 2021 08:07 UTC
  • Magaidi 100 wa Al Qaida wauawa katika mpaka wa Burkina Faso na Mali

Mamluki 100 wenye mfungamano na kundi la kigaidi la al Qaida wameuawa katika oparesheni za pamoja kati ya Burkina Faso na Niger katika mpaka wa nchi mbili hizo.

Jeshi la Burkina Faso jana usiku lilitangaza kuwa magaidi hao waliuawa katika oparesheni za pamoja ya nchi mbili hizo kuanzia Novemba 25 hadi tarehe 9 mwezi huu wa Disemba. Mamia ya wanajeshi katika mpaka wa pamoja wa Niger na Burkina Faso walishiriki katika oparesheni hizo za pamoja. 

Ripoti zinasema kuwa katiak oparesheni hizo za pamoja za majeshi ya Niger na Burkina Faso watu 20 wakiwa na silaha, zana za kijeshi na mamia ya pikipiki walitiwa mbaroni na mada za milipuko 15 pia ziliharibiwa. 

Burkina Faso, Mali na Niger kwa miaka kadhaa sasa zinatatizwa na mashambulizi na hujuma za makundi ya kigaidi. Aidha kuanzia mwaka 2015 hadi sasa mapigano na mashambulizi ya kigaidi yamesababisha kuuliwa zaidi ya watu 1200 na wengine zaidi ya milioni moja kuwa wakimbizi. 

Wakimbizi wa Burkina Faso na Mali 

Umoja wa Mataifa umearifu kuwa magaidi waliopo magharibi mwa Afrika mwaka 2019 walisababisha vifo vya watu 4000 kupitia hujuma na mashambulizi dhidi ya raia katika maeneo mbalimbali.

Tags