Jan 17, 2022 02:38 UTC
  • Mjumbe Maalumu wa UN Libya: Kipaumbele kikuu ni maridhiano ya kitaifa

Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amesema kuwa, kipaumbeke kikuu zaidi hivi sasa kuhusu Libya ni kuweko maridhiano ya kitaifa na kusisitiza kuwa wananchi wa Libya hawataki tena vita.

Bi Stephanie Williams ambaye alielekea Cairo mji mkuu wa Misri kwa lengo la kushauriana na kuchunguza njia za kuunga mkono suala la kufanyika uchaguzi huko Libya amesisitiza kuwa, kuna haja ya kutchukuliwa hatua za dhati ili kufanikisha mapatano ya kitaifa nchini Libya.

Amesema, jukumu kuu katika uwanja huo linamhusu Rais wa nchi.  

Williams ameashiria hamu ya pande zinazozozana huko Libya kwa ajili ya mazungumzo na kuongeza kuwa, Umoja wa Mataifa itakuwa bega kwa bega na Libya kwa ajili ya kufikia maridhiano ya kitaifa na kuitisha uchaguzi.

Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Libya inapasa kutoa uzito kwa suala kuu la kufanyika uchaguzi. 

Wananchi wa Libya wanataraji kuwa chaguzi za Bunge na Rais nchini humo zitasaidia jitihada za kuhitimisha mapigano yaliyoiathiri nchi hiyo kwa miaka kadhaa sasa.

Wanamgambo wenye silaha huko Libya

 

Tags