Jan 23, 2022 12:18 UTC
  • Viongozi wa Sudan na Ethiopia wakutana kujadili uhusiano wa nchi zao uliozorota

Kiongozi nambari mbili mwenye nguvu nchini Sudan amekutana kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Ethiopia katika ziara ya nadra mjini Addis Ababa kufanywa na afisa kutoka Khartoum.

Mohamed Hamdan Daglo, anayejulikana sana kama Hemeti, ambaye ni kiongozi nambari mbili katika baraza la uongozi la Sudan, alitarajiwa kuwepo nchini Ethiopia kwa siku mbili na atakutana na maafisa kadhaa wa Ethiopia. Taarifa zaidi zinasema kuwa, kiongozi huyo amekutana na kufanya mazungumzo pia na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Uhusiano kati ya Khartoum na Addis Ababa umezorota kutokana na vita vya eneo juu mzozo wa mpaka wa mkoa wa Al-Fashaga, ambako wakulima wa Ethiopia wanalima katika ardhi yenye rutuba ambayo Sudan wanadai ni mali yao.

Hivi karibuni serikali ya Ethiopia ilitangaza kuwa imekubali upatanishi wa nchi nyingine katika mgogoro baina yake na nchi jirani ya Sudan lakini kwa masharti.

Mzozo wa mpaka baina ya Sudan na Ethiopia umekuwa ukitishia mustakabali wa uhusiano baina ya nchi mbili hizi

 

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ethiopia, Dina Mufti amenukkuuliwa mara kadhhaa akitaka serikali ya Sudan ikomeshe mashambulizi na kuwafukuza raia wa Ethiopia katika maeneo yao katika operesheni zilizoanza tarehe 6 Novemba 2020 wakati Addis Ababa ilipokuwa ikirejesha utawala wa sheria katika eneo la Tigray.

Nchi mbili za Sudan na Ethiopia zimekuwa zikituhumiana kushambulia na kukalia kwa mabavu ardhi ya kila mmoja wao, tuhuma ambazo zinatishia mustakabali wa uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili. Sudan na Ethiopia zimekuuwa zikkivutana pia kuhusiana na kadhia ya ujenzi wa Bwawa la al-Nahdha.