Jan 25, 2022 11:47 UTC
  • Watu wasiopungua 8 waaga dunia kaika msongamano, mechi ya mpira wa miguu AFCON

Msongamano mkubwa wa watu watu katika uwanja wa mpira wa miguu wa Paul Biya mjini Yaounde umesababisha vifo vya watu wasiopungua 8 na kujeruhi makumi ya wengine.

Tukio hilo lilijiri wakati wa mechi ya kandanda kati ya timu ya taifa ya Cameroon, mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na timu ya taifa ya Comoro. Picha za video zinaonyesha mashabiki waking'ang'ana kuingia kwa nguvu katika uwanja Paul Biya uliopo katika mji mkuu, Yaounde.

Maafisa wa Cameroon wamesema kuwa, watu karibu elfu hamisini walikuwepo uwanjani hapo kwa ajili ya kutazama mechi hiyo ya mpira wa miguu.

Gavana wa jimbo la kati la Cameroon Naseri Paul Biya, amesema kuwa huenda kukawa na idadi zaidi ya wahanga. 

Ripoti nyingine imesema kuwa watoto kadhaa walijeruhiwa na kupoteza fahamu katika tukio hilo.

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limesema katika taarifa yake kwamba kwa sasa "linachunguza tukio hilo na kujaribu kupata taarifa zaidi za kile kilichotukia".

Timu ya taifa ya Cameroon imeichapa Comoro mabao mawili kwa moja.