Jan 26, 2022 04:13 UTC
  • Msafara wa misaada ya kibinadamu kuelekea Tigray wazuiwa

Duru zinazohusika na masuala ya kibinadamu nchini Ethiopia zimeripoti kuwa msafara wa misaada ya kibiandamu iliyokuwa ikipelekwa Tigray kaskazini mwa Ethiopia imezuiliwa.

Duru hizo zimeeleza kuwa, malori yanayobeba misaada ya  vyakula na mahitajio muhimu kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo lililoathiriwa na vita yalisimamishwa jana Jumanne katika kituo cha upekuzi katika eneo la Afar kaskazini mwa Ethiopi na haijulikani iwapo malori hayo yataruhusiwa kuendelea na safari au la.  

Kila upande kkati yya Serikali ya Ethiopia na Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray (TPLF) kila moja inautuhumu upande wa pili kuwa chanzo cha hali inayoshuhudiwa sasa katika eneo la Tigray. Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) umeeleza kuwa, malori 27 yanayobeba tani 800 za chakula Jumapili iliyopita yalianza safari kutoka eneo la Afar kuelekea Mekelle, makao makuu ya eneo la Tigray. 

Wiki iliyopita pia Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa ugawaji wa chakula huko Tigray umepungua sana na kufikia kiwango cha chini na kwamba mapigano yanayoendelea katika eneo hilo yanawafanya mamia ya maelfu ya watu kuishi katika mazingira magumu. 

Wakimbizi katika eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Novemba 4 mwaka juzi wa 2020 alitoa amri ya kushambuliwa eneo la Tigray baada ya kuituhumu harakati ya TPLF kuwa imevishambulia vikosi vya jeshi la serikali. Mapigano huko Tigray hadi sasa yamewalazimisha raia karibu milioni mbili kuwa wakimbizi na wengine laki nne kukabiliwa na njaa. 

Tags