Jan 29, 2022 03:21 UTC
  • Shirika la misaada: Kuendelea ukame kutasababisha vifo na watu kulazimika makwao Somalia

Shirika la utoaji misaada ya kibinadamu la Norway Refugee Council (NRC) mjini Mogadishu nchini Somalia limeonya kuwa huenda watu kadhaa wakapoteza maisha huku wengine zaidi ya milioni 1 wakalazimika kuhama makwao kutokana na hali ya ukame kuendelea kuwa mbaya nchini humo.

Kulingana na shirika hilo la misaada, kwa sasa raia wa Somalia wapatao laki 2 na elfu 45 wamelazimika kuhama makwao kutokana na ukame, huku idadi hiyo ikikadiriwa kuongezeka hadi milioni 1.4 mwaka huu wa 2022 kutokana na hali hiyo kuendelea kuwa mbaya zaidi katika maeneo kadhaa nchini humo.

Takriban watu milioni 3.2 idadi ambayo ni sawa na theluthi moja ya watu wote nchini humo wameathirika na ukame hali ambayo inawaweka katika hatari ya kukumbwa na njaa, utapia mlo na kupanda kwa bei za bidhaa pamoja na kupoteza mimea na mifugo yao.

Raia wa Somalia walioathiriwa na ukame

Aidha NRC inasema, wafanyakazi wake wameripoti ongezeko la vifo vinavyohusishwa na ukame, watoto wanaokumbwa na utapiamlo na watu  kutafuta misaada.

Mkurugenzi wa  shirika hilo la misaada nchini Somalia, Mohammed Abdi ametoa wito kwa nchi wafadhili kuchanga fedha zitakazosaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu walioathirika na ukame nchini humo.../

Tags