Apr 07, 2022 01:55 UTC
  • Blaise Compaore
    Blaise Compaore

Rais wa zamani wa Burkina Faso amehukumiwa kifungo cha maisha jela katika kesi ya mauaji ya Thomas Sankara, kiongozi wa mapinduzi wa nchi hiyo na shujaa wa bara la Afrika yaliyotekelezwa mwaka 1987.

Hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, ilisomwa jana Jumatano na Mahakama ya Kijeshi na imehitimisha kesi ya mauaji ya rais wa zamani wa Burkina Faso, ambayo ilianza kusikilizwa miezi sita iliyopita.

Waendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kijeshi iliyoko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso walikuwa wameitaka korti imhukumu Campaore na washukiwa wenzake 13 kifungo cha miaka 30 jela. 

Kesi ya 14 hao akiwemo rafiki wake za zamani yaani Blaise Compaore ambaye alishika hatamu za uongozi huko Burkina Faso baada ya kuaga dunia Thomas Sankara na kudumu madarakani kwa miaka 27, ilianza kusikilizwa Oktoba mwaka jana 2021 katika mji mkuu wa nchi hiyo Ouagadougou.

Thomas Sankara ambaye alipewa jina la Che Guevara wa Afrika alipigania suala la kufuta fikra za kikoloni, kukomesha ukandamizaji na kuwa huru wananchi wa Burkina Faso na barani Afrika kwa ujumla.

Thomas Sankara

Hata hivyo ndoto zake za kimapinduzi zilifupishwa pale alipouawa kwa kupigwa risasi katika mapinduzi ya mwaka 1987, miaka minne baada ya kuingia madarakani. 

Mwamajimui huyo wa Afrika ambaye aliingia madarakani mwaka 1983, aliuawa akiwa na umri wa miaka 37, akiwa pamoja na maafisa wengine 12 wa serikali.

 

Tags