Apr 22, 2022 07:55 UTC
  • Maambukizi ya UVIKO-19 yaongezeka Afrika Kusini

Afrika Kusini ambayo ilikuwa shwari kutokana na kupungua kwa maambukizi ya corona kwa kiasi fulani katika siku za karibuni imetangaza kukumbwa kwa mara nyingine tena na ongezeko la maambukizi ya corona nchini humo.

Afrika Kusini imesajili zaidi ya maambukizi milioni 3 na 750,000 ya UVIKO-19  na vifo zaidi ya laki moja na 270. Shirika la habari la Ufaransa leo limeripoti kuwa, maafisa wa afya wa serikali ya Afrika Kusini katika muda wa saa 24 zilizopita wamesajili kesi mpya za corona 4,406.

Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Kuambukiza ya Afrika Kusini pia imetoa taarifa na kueleza kuwa watu hao 4,406 waliripotiwa kuwa na maambukizi ya corona jana Alhamisi. 

Kwa mujibu wa takwimu hizo, maambukizi ya corona nchini Afrika Kusini yanaonyesha kuongezeka kwa asilimia 15.8. Aidha idadi ya wagonjwa wanaokwenda hospitali kwa matibabu pia imeongezeka hata hivyo vifo vinavyotokana na corona havijaongezeka. 

Afrika Kusini mwanzoni mwa mwezi Machi mwaka huu ilipitisha duru ya masaa 48  bila ya kuripoti kifo chochote kutokana na maambukizi ya corona; maambukizi ambayo yaliiathiri pakubwa nchi hiyo tokea mwaka 2020. 

UVIKO-19 iliposhika kasi Afrika Kusini mwaka 2020 

 

Tags