Apr 23, 2022 07:26 UTC
  • Mali yagundua kaburi la umati kwenye kambi ya zamani ya kijeshi ya Ufaransa

Jeshi la Mali limetangaza kuwa, limegundua kaburi la umati kwenye kambi ya zamani ya kijeshi ya Ufaransa katika eneo la Gossi la kaskazini mwa nchi hiyo.

Jeshi la Ufaransa lililazimika kuondoka kwenye kambi hiyo mwezi Februari mwaka huu baada ya jeshi la Mali kumlaumu mkoloni huyo kizee wa Ulaya kwamba anashiriki katika kuharibu usalama wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. 

Ufaransa inadai kwamba watu iliowaita mamluki wa Russia wametengeneza kwa makusudi kaburi hilo la umati ili kuitupia lawama Ufaransa.  Lakini serikali ya Mali imekanusha vikali madai ya Ufaransa kuwa, mamluki wa Russia wametengeneza kwa makusudi kaburi hilo la umati ikiwa ni ishara ya wazi kuwa serikali hiyo ya Bamako inaamini kwamba wanajeshi wa Ufaransa ndio waliofanya mauaji hayo ya umati.

Wanajeshi vamizi wa Ufaransa nchini Mali

 

Jeshi la Mali limetangaza kuwa, kaburi hilo la umati limepatikana karibu mno na kambi ya kijeshi ya Barkhane iliyokuwa inakaliwa kwa mabavu na Wafaransa kaskazini mwa Mali.

Uchunguzi haraka kuhusu kaburi hilo la umati lililogunduliwa kwenye kambi ya kijeshi iliyokuwa ikidhibitiwa na wanajeshi wa mkoloni Ufaransa kabla hawajatimuliwa huko Mali tayari umeanza.

Hasira za wananchi wa nchi za magharibi mwa Afrika kama Mali na Burkina Faso dhidi ya mkoloni Mfaransa ni kubwa na zinaonengezeka siku baada ya siku wakimlaumu mkoloni huyo wa Ulaya kwa kushirikiana na magenge ya kigaidi kuhatarisha usalama wa nchi hizo na kuingilia mambo yao ya ndani. 

Wananchi wa Burkina Faso kwa mfano waliwahi kuisimamisha mara kadhaa misafara ya kijeshi ya Ufaransa wakiishutumu kuwa inahamisha magaidi kuwapeleka sehemu nyingine kwa ajili ya kufanya vitendo vya kigaidi.

Tags