May 04, 2022 08:05 UTC
  • Abdulhamid al-Dbeibah
    Abdulhamid al-Dbeibah

Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amesema kuwa, wananchi wa Libya hawana njia nyingine isipokuwa kuitisha uchaguzi na amesisitiza kuwa anafungamana na chaguzi za Bunge na Rais wa nchi hiyo.

Libya imetumbukia katika mgogoro wa kisiasa kutokana na kukosekana umoja miongoni mwa taasisi ya jeshi na nafasi za uongozi wa serikali na sasa nchi hiyo iko katika ombwe la kisiasa kwa sababu ya hitilafu za mitazamo kati ya makundi ya ndani. 

Makundi ya kisiasa yakumbwa na hitilafu za kimitazamo 

Jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa zinaamini kuwa, njia pekee ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa sasa wa Libya ni kufanyika chaguzi wa Bunge na Rais nchini humo.  

Abdulhamid al-Dbeibah Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya nchi hiyo aidha ametangaza kuwa, ni rahisi kuendesha chaguzi hizo mbili na tayari sheria na kanuni zake zimeshatungwa.

Uchaguzi wa rais na bunge utafanyika tu huko Libya haijalishi wapangaji njama wanafanya mikakati kiasi gani. 

al-Dbeibah amekataa kukabidhi mamlaka kwa serikali mpya, akisema kuwa atakabidhi madaraka kwa waziri mkuu aliyechaguliwa kwa kura za wananchi. 

Itakumbukwa kuwa, mnamo Februari 10, 2022, Bunge la Libya lilimchagua Fathi Bashagha kuwa Waziri Mkuu mpya na kuchukua nafasi ya Abdulhamid al-Dbeibah.

Tags