May 08, 2022 02:43 UTC
  • Indhari ya Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro mkubwa wa chakula Afrika

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa kupanda pakubwa bei ya chakula na mafuta kutokana na vita vya Ukraine, kumeibua mgogoro mkubwa wa chakula barani Afrika ambao haujawahi kushuhudiwa.

Mapigano huko Ukraine na vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Moscow yametatiza usambazaji wa ngano, mbolea za kemikali na bidhaa zingine; jambo ambalo limeibua matatizo zaidi kwa Afrika. Raymond Gilpin mchumi wa ngazi ya juu wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa barani Afrika anasema kuhusiana na hili kwamba: Mgogoro huu mkubwa umeliathiri bara la Afrika. Tunashuhudia kushuka kwa mapato ya ndani katika nchi za bara la Afrika." Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa imefika milioni 193 na karibu wengine milioni 40 pia wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula. Kwa msingi huo, Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Yemen na Afghanistan ndio walioathirika pakubwa na njaa na uhaba wa chakula kati ya nchi 53 ambazo zimekumbwa na mgogoro huo wa chakula.  

Wakati huo huo mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi, taathira za maambukizi ya UVIKO-19 na kuongezeka ukosefu wa amani ambao ni natiga ya hujuma na mashambulizi ya makundi ya kigaidi, ni sababu kuu tatu ambazo katika miaka ya karibuni zimedisha matatizo ya kiuchumi, kijamii, umaskini na ukosefu wa ajira na kuzitatiza zaidi nchi mbalimbali khususan nchi za Kiafrika. Baadhi ya maeneo ya Kenya, Ethiopia na Somalia yamekumbwa na ukame mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 40 iliyopita. Hata kama mashirika ya misaada ya kibinadamu yanafanya juhudi za kuzuia kutokea tena njaa na ukosefu wa chakula kama ule ulioshuhudiwa muongo mmoja uliopita ambao uliuwa mamia ya maelfu ya watu lakini taasisi hizo zina sehemu ndogo sana ya bajeti inayohitajika kukabiliana na janga hilo la ukame. 

Ukame Somalia 

Mohamed Adow Mkuu wa Taasisi ya Power Shift Africa anasema kuhusiana na hili kuwa: Baadhi ya nchi maskini sana duniani zimelazimika kustafidi na rasmilimali adimu kukabiliana na mgogoro huo ambao hazihusiki katika kuuanzisha. Nchi hizo pamoaj na kuwa hazihusiki hata kidgogo katika kusababisha hewa chafu ya carbon kulinganisha na nchi tajiri duniani lakini ni waathirika wakuu wa ukame, vimbunga na majanga  ya mafuriko yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.  

Hii ni katika hali ambayo, vita vya Ukraine vimeshadidisha hali mbaya ya uchumi na ukosefu wa chakula katika nchi za Kiafrika; sawa kabisa na kama alivyotahadharisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala kwamba: Vita vya Ukraine vimeathiri pakubwa bei za bidhaa za vyakula na kusababisha upungufu wa chakula; jambo linaloweza kusababisha ukosefu wa chakula katika nchi maskini duniani. 

Ngozi Okonjo- Iweala, Mkurugenzi Mkuu wa WTO 

Karibu robo ya ngano duniani inatoka Russia na Ukraine huku asilimia 40 ya ngano na mahindi ya Ukraine yakiuzwa katika nchi za Asia Magharibi na barani Afrika. Kuhusiana na suala hilo, nchi za mashariki mwa Afrika zinanunua asilimia 80 ya ngano inazohitajia kutoka Ukraine na Russia. Hii ni katika hali ambayo, bei ya ngano kimataifa imeongezeka sana sawa kabisa na ilivyokuwa wakati wa mgogoro wa fedha duniani mwaka 2008; kiasi kwamba hatari ya njaa sasa imekuwa kubwa katika akthari ya nchi duniani. 

Afrika Mashariki hununua asilimia 80 ya ngano kutoka Russia na Ukraine 

Katika hali ambayo, nchi za Ulaya na Marekani zimeipatia Ukraine sehemu kubwa ya bajeti na suhula zao ili kuidhaminia nchi hiyo silaha na zana za kijeshi huku zikichochea moto wa vita kati ya Russia na nchi hiyo; taathira za vita hivyo pia sasa zinazisibu pakubwa nchi maskini duniani zikiwemo baadhi ya nchi barani Afrika. Ukweli ni kuwa, nchi za Magharibi pia zimezifanya nchi maskini wahanga wa sera zao sawa kabisa na kama zilivyofanya katika janga la UVIKO-19 ambapo hazikuzipatia nchi hizo chanjo za kukabiliana na corona; hatua ambayo ni kinyume na majukumu ya nchi hizo kimataifa. Kuhusiana na hilo, Mkurugenzi Mkuu wa wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) amezitahadharisha nchi wazalishaji wa bidhaa za chakula kuhusu kujilimbikizia bidhaa na kueleza kuwa, ni muhimu sana kujiepusha na kukaririwa tajiriba ya janga la corona. Ni dhahir shahir kuwa, nchi za Kiafrika  sasa ni wahanga wakubwa wa sera za kupenda vita za nchi za Magharibi.  

 

Tags