May 09, 2022 07:48 UTC
  • Bei ya petroli yaongezeka pakubwa nchini Ethiopia

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Kikanda ya Ethiopia imetangaza ongezeko la asilimia 16 la bei ya petroli katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Bei ya mafuta duniani imefikia kiwango cha juu kabisa tangu mwaka 2008 ambapo kwa sasa pipa moja la mafuta linauzwa kwa zaidi ya dola 100 na hilo ni kutokana na hofu ya kuwepo upungufu wa bidhaa hiyo muhimu katika masoko ya kimataifa kufuatia operesheni ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Kikanda ya Ethiopia imesema katika taarifa yake kwamba bei ya petroli kwa lita moja ya itaongezeka kutoka Birr 31.74 (sarafu ya Ethiopia) hadi Birr 36.87.

Baada ya kuongezeka bei ya gesi, bei ya dizeli pia imeongezeka kwa kiwango kikubwa nchini humo.

Kituo cha petroli

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Kikanda ya Ethiopia imehusisha kupanda kwa bei ya mafuta nchini na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu katika masoko ya kimataifa. Kulingana na Ofisi Kuu ya Takwimu ya Ethiopia, mfumuko wa bei ulipanda kwa asilimia 2.1 mwezi Aprili kutoka asilimia 36.6 mwezi Machi.

Bei ya Shirika la Nchi Zinazouza Petroli kwa Wingi Duniani (OPEC) imeongezeka kwa dola 2 na senti 21 kwa pipa ambapo leo, Jumatatu, linauzwa kwa dola 113 na senti 4.

Viongozi wa nchi wanachama wa kundi la G7 walitoa taarifa ya pamoja jana (Jumapili) na kuahidi kusimamisha hatua kwa hatua utegemezi wao kwa nishati ya Russia, ikiwa ni pamoja na mafuta.

Tags