May 10, 2022 08:56 UTC
  • Kuendelea ukosoaji wa Algeria wa mauaji ya kinyama ya Ufaransa dhidi ya Waalgeria

Licha ya kupita miongo kadhaa tangu Ufaransa ifanyye mauaji ya kinyama dhidi ya wananchi wa Algeria, lakini mafaili ya jinai hiyo yangali wazi na yanaweza kufuatiliwa.

Akihutubia kwa mnasaba wa kumbukumbuu ya mwaka wa 78 wa mauaji ya Mei mwaka 1945 yaliyofanywa na jeshi la mkoloni Mfaransa, Rais Abdelmajid Tebboune wa Algeria sanjari na kulaani mauaji hayo yya kinyama amesisitiza kwamba, Algeria haitalegeza kamba kwa namna yoyote ile kuhusiana na mafaili ya kipindi hicho cha mkoloni Mfaransa na kwamba, itafuatilia kadhia hiyo kwa nguvu zake zote.

Rais Tebboune amegusia kwa kusema kuwa, jinai hiyo ingali katika kumbukumbu za wananchi wa Algeria na kueleza kwamba, mauaji ya kinyama ya Wafaransa nchini Algeria ni kitu ambacho katu hakiwezi kusahauliwa. Kadhalika amesema, vikosi vamizi wa Ufaransa katika zama hizo viliuawa kwa umati waandamanaji.

Ufaransa ilikoloni Algeria kwa miaka 132 yaani kuanzia mwaka 1954 hadi 1962. Hatimaye nchi hiyo mwaka 1962 ikapata uhuru baada ya miaka kadhaa ya mapambano ya ukombozi ya umwagaji damu ambapo zaidi ya Waalgeria milioni moja waliuawa na majeshi ya mkoloni Mfaransa.

Katika zama hizo Ufaransa ilifanya majaribio ya nyuklia katika baadhi ya maeneo ya Algeria na kuwaambukiza mionzi ya nyukilia watu wa vijiji vilivyokuweko kandokando ya eneo la majaribio hayo kwa lengo la kutaka kufahamu taathira za nyuklia kwa wanadamu.

Jinai za Mkoloni Mfaransa nchini Algeria

 

Jinai za Wafaransa zilikuwa kubwa kiasi kwamba, kiwango kikubwa cha taka zilizoachwa na majaribio hayo ya nyuklia ambazo zina muda mrefu sana zikiwa katika mnururiko wa nyuklia zingali zinaonekana juu ya ardhi ya Algeria na nyingine zimezikwa chini ya ardhi.

Abdul-Majid Sheikhi, mshauri wa masuala ya kihistoria wa Rais wa Algeria ameashiria jinai mbalimbali za Wafaransa katika zama za ukoloni na kusema kuwa: Wakoloni hao walikuwa wakitumia hata mifupa ya wanamapambano wa Algeria kwa ajili ya kutengeneza sabuni na kusafisha sukari, kiasi kwamba, mifupa mingi ya wahanga wa jinai za Wafaransa ilisafirishwa na kupelekwa katika mji wa Marseille nchini Ufaransa.

Jinai za Wafaransa nchini Algeria ni mashuhuri kiasi kwamba, hivi karibuni hata Rais Emmanuel Macron alilazimika kukiri kutokea jinai hizo na kuuonyesha umma nyaraka zinazohusiana na majaribio ya nyuklia ya Ufaransa nchini Algeria.

Kuhusiana na hilo, Rais Abdelmajid Tebboune wa Algeria amesema kuwa, wakoloni wa Kifaransa hakuna walichoiletea Algeria ghairi ya uharibifu na kusisitiza kuwa, faili la jinai za Wafaransa katika nchi hiyo ya Kiafrika linapaswa kuchunguwa kwa insafu, uadilifu na uwazi.

Katika miaka ya hivi karibuni viongozi wa Algeria na Ufaransa wamefanya mazungumzo mara chungu nzima kujadili jinai za Wafaransa katika zama za ukoloni huko Algeria, na takwa kuu la viongozi wa Algiers ni Ufaransa kuomba radhi rasmi na kuilipa fidia nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo, viongozi wa Ufaransa kila mara wamekuwa wakiamiliana na takwa hili kwa mbinu na njia tofauti kulingana na mazingira na anga ya kisiasa ya nchi hiyo ya bara Ulaya. Kuna wakati viongozi hao wamekuwa wakikiri kutokea jinai hiyo lakini husema kuwa, hawawezi kuomba radhi. Aidha wakati mwingine wanakana kutokea jinai hizo na kulikabidhi hilo kwa historia. Misimamo na matamshi haya yasiyo na uratibu yamekuwa yakizorotesha uhusiano wa Ufaransa na Algeria.

Xavier Driencourt, balozi wa zamani wa Ufaransa nchini Algeria amekosoa vikali utendaji wa sasa wa serikali ya Paris mkabala na Algeria na kusisitiza kwamba, baada ya kupita miaka 60 tangu Algeria ipate uhuru, kama Ufaransa inataka kurekebisha makosa yake ya huku nyuma katika nchi hiyo ya Kiarafrika na hivyo kuwa na uhusiano wenye uwiano, inapaswa kuchukua maamuzi ya kishujaa zaidi kuhusiana na nchi hiyo.

Hata hivyo jinai za Ufaransa barani Afrika hazikuishia kwa Algeria tu, bali kaumu, mbari na mataifa mengi ya Kiafrika nayo yalikuwa wahanga wa jinai za Wafaransa.

Marais wa Ufaransa na Algeria

 

Katika mauaji ya kimbari ya Rwanda yaliyotokea mwaka 1994, mauaji ya Mali au jinai zilizotokea katika mataifa mengine ya Kiafrika ya eneo la Sahel Afrika, daima nyayo za Ufaransa zimekuwa zikionekana. Filihali Ufaransa ikiwa katika kalibu ya ukoloni mpya imeendelea kuweko katika maeneo mbalimbali barani Afrika ikiwa imevaa mavazi kama mtoaji wa misaada ya kibinadamu, muendeshai vita dhidi ya ugaidi au kutumia kisingizio kama cha kusaidia kurejesha amani na usalama.

Pamoja na hayo, uwepo wa majeshi ya Ufaransa katika maeneo hayo, haujawa na matunda yoyote kwa mataifa hayo ghairi ya kuyaongezea matatizo. Alaa kulli haal, filihali Rais wa Algeria kwa mara nyingine tena sambamba na kukumbusha jinai za Ufaransa amesisitiza kuwa, mafaili yanayohusiana na kipindi cha mkoloni Mfaransa nchini Algeria yatashughulikiwa na kufuatilia pasi na ya kuweko muamala au ulegezaji kamba suala linaloonyesha kwamba, haionekani kama Ufaransa itakubaliana na hilo.

Tags