May 17, 2022 07:33 UTC
  • Marekani kutuma wanajeshi Somalia kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la al Shabab

Katika kuendeleza hatua zake za kijeshi na sera za uingliaji kati , Rais Joe Biden wa Marekani amesema kuwa washington ina mpango wa kutuma tena wanajeshi wa nchi hiyo huko Somalia kwa lengo la kile alichokitaka kuwa kupambana na kundi la kigaidi la al Shabab lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, afisa wa ngazi ya juu wa Marekani amedai kuwa Rais Joe wa Biden wa nchi hiyo amekubali ombi la Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo akitaka wanajeshi wa Marekani watumwe tena Somalia. Amesema wametaka vikosi vya Marekani vitumwe tena huko Somalia ili viweze kupambana vyema dhidi ya wanamgambo wa al Shabab ambao wamejizatiti hivi sasa na kuwa tishio kubwa. 

Afisa huyo wa ngazi ya juu wa Marekani ameendelea kudai kuwa hayo ni mabadilishano tu ya wanajeshi ambao walikuwepo katika eneo hulo huko nyuma. Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump mwezi Januari mwaka jana aliamua kuwaondoa wanajeshi wa nchi hiyo waliokuwepo Somalia. 

Al Shabab ni kundi lenye silaha na la kigaidi lenye mahusiano na mtandao wa al Qaida; ambalo limehusika katika oparesheni nyingi za kigaidi zilizouwa na kujeruhi mamia ya watu katika nchi mbalimbali barani Afrika. 

Hujuma za uharibifu za kundi la al Shabab, Mogadishu 

Al Shabab mara kadhaa limetekeleza mashambulizi na hujuma za uharibifu dhidi ya vikosi vya serikali na askari jeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu sambamba na kutekeleza oparesheni kadhaa za umwagaji damu katika maeneo mbalimbali barani Afrika. 

 

Tags