May 17, 2022 09:08 UTC
  • Kufichuliwa jinai za Ufaransa baada ya kugunduliwa makaburi ya umati nchini Mali

Kugunduliwa makaburi ya umati jirani na kambi ya jeshi ya Ufaransa nchini Mali kumezidi kuweka wazi siku baada ya siku ukubwa wa jinai za Wafaransa katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Wananchi wengi wa Mali wameandamana na kuitaka Ufaransa itoe maelezo kuhusiana na mkasa wa makaburi hayo ya umati jirani na kambi ya jeshi ya Ufaransa katika eneo la Gossi la kaskazini mwa nchi hiyo.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walisikika wakipiga nara dhidi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Baadhi ya mabango hayo yalikuwa na maandishi yasemayo: "Macron ni chinjachinja wa Gossi."

Hivi karibuni jeshi la Mali lilitangaza kuwa, limegundua kaburi la umati kwenye kambi ya zamani ya kijeshi ya Ufaransa katika eneo la Gossi la kaskazini mwa nchi hiyo. Baada ya kugunduliwa makaburi hayo ya umati, wanajeshi wa Mali walielekeza tuhuma kwa vikosi vya Ufaransa kwamba, vimefanya mauaji ya umati dhidi ya raia wa nchi hiyo ya Kiafrika.

Uchunguzi haraka kuhusu kaburi hilo la umati lililogunduliwa kwenye kambi ya kijeshi iliyokuwa ikidhibitiwa na wanajeshi wa mkoloni Ufaransa kabla hawajatimuliwa huko Mali tayari umeanza.

Hii ni katika hali ambayo, mwanzoni mwa mwezi uliopita wa Aprili, Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch, lililituhumu jeshi la Mali na askari wa kigeni walioko nchini humo kwamba, wamefanya mauaji ya raia wapatao 300 ambao hawakuwa na hatia yoyote.

Wanajeshi wa Mali nchini Ufaransa

 

Katika tuhuma nyingine, Idara ya Mahakama ya Mali ilimuita Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa. Le Drian aliitwa na kukabidhiwa malalamiko kadhaa hususan katika fremu ya uchunguzi wa hasara kwa mali za umma.

Katika miaka ya hivi karibuni Ufaransa imekuwa na uwepo na mahudhurio amilifu katika akthari ya mataifa ya Kiafrika hususan mataifa ya Ukanda wa Eneo la Sahel Afrika na imekuwa ikitumia visingizio mbalimbali kuhalalisdha uwepo wake wa kijeshi kama kupambana na ugaidi na kusaidia juhudi za kurejesha amani na usalama katika maeneo hayo.

Vikosi vya Ufaransa viko nchini Mali, Chad na katika mataifa mengine ya Kiafrika. Hata hivyo kabla ya majeshi hayo kufanya mambo kwa mujibu wa madai yanayotolewa na Paris yamekuwa yakifanya mambo katika fremu ya malengo ya kiuchumi na kisiasa ya Ufaransa. Ukweli wa mambo ni kuwa, katika karne za hivi karibuni Ufaransa imetenda jinai nyingi katika mataifa ya Algeria, Rwanda na katika baadhi ya nchi za Kiafrika. Katika miongo ya hivi karibuni Ufaransa imebadilisha mbinu na mikakati yake na kuonyesha sura mpya ya ukoloni barani Afrika.

Uhakika wa mambo ni kuwa, viongozi wa Ufaransa wanadai kwamba, ni wenye kuwasaidia watu wa Afrika, katika hali ambayo, kinachoonekana ni jinai, mauaji na kupora mali za mataifa ya bara hilo suala ambalo linaonyesha ni kwa kiasi gani Wafaransa wanatenda dhulma dhidi ya Waafrika.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa

 

Kusaidia kuvuruga utulivu wa kisiasa, kuunga mkono mapinduuzi ya kijeshi na uasi wa kisilaha katika nchi za Niger, Guinea, Libya, Mali, Burkina Faso na kwingineko ni mifano mingine ya wazi kabisa ya uingiliaji wa Ufaransa na washirika wake katika mataifa ya Kiafarika hususan katika nchi zilizoko katika Ukanda wa Sahel Afrika. Hii ni kutokana na kuwa, nchi za eneo la Sahel Afrika zina nafasi muhimu ya kijiopolitiki barani Afrika na akthari yazo zimekuwa zikizingatiwa na kukodolewa macho ya tamaa na Ufaransa na waitifaki wake kutokana na kuwa na vyanzo vya utajiri na nafasi ya kijiografia zilizo nayo.

Majuzi mamia ya wananchi wa Chad waliandama na kulalamikia uwepo wa vikosi vya Ufaransa katika nchi yao. Waandamanaji hao wenye hasira walisikika wakipiga nara kama: "Ufaransa toka nje" na " Hapana, hatutaki ukoloni". Si hayo tu, bali waliharibu vituo kadhaa vya mafuta vya Shirika la Kimataifa la Mafuta la Total ambalo ni nembo ya Ufaransa.

Majaribio ya nyuklia ya Ufaransa katika kipindi cha ukoloni nchini Algeria ambayo yamesababisha maafa makubwa

 

Kituo cha Utafiti wa Kistratejia Afrika kimetangaza katika ripoti yake kwamba, kufuatia uingiliaji wa kigeni barani Afrika, matukio ya utumiaji mabavu yanayohusishwa na makundi ya kigaidi katika nchi za eneo la Sahel Afrika yameongezeka kwa asilimia 70 na hivyo kuepelekea kusajiliwa rekodi mpya ya matukio ya vitendo vya utumiaji mabavu vya kufurutu ada barani Afrika katika mwaka uliopita wa 2021.

Licha ya kuwa, Ufaransa imetangaza kuwa, itaondoa vikosi vyake vya kijeshi nchini Mali, lakini viongozi wa Paris wamekiri kwamba, nchi yao haitaondoka Afrika. Inaonekana kuwa, Ufaransa na washirika wake licha ya kufanya jinai zote hizo na licha ya kuweko matakwa ya wananchi wa bara hilo ya kuondoka katika mataifa yao, hawako tayari kufumbia macho hata kidogo maslahi yao barani humo.

Tags