May 20, 2022 07:30 UTC
  • Rwanda : Awamu ya kwanza ya wahamiaji kutoka Uingereza watawasili hivi karibuni

Waziri mkuu wa Rwanda, Edouard Ngirente, amesema awamu ya kwanza ya wahamiaji kutoka nchini Uingereza, watawasili huko Rwanda hivi karibuni, na kwamba nchi hiyo imekamilisha matayarisho ya kuwapokea.

Ngirente amesisitiza kuwa mpango huo kati ya  Rwanda na Uingereza una malengo mazuri huku akiwapuuza wanaokosoa mpango huo ambao utagharimu dola milioni 120, huku baadhi ya watafuta hifadhi wakitarajiwa kusafirishwa hadi taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mashirika ya kiraia yamekosoa vikali hatua hiyo ya serikali ya Rwanda na kuitaja kuwa isiyofaa na ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Hata hivyo Ngirente amesema mashirika hayo yatapongeza mpango huo pindi baada ya kutekelezwa kikamilifu.

Edouard Ngirente

Tayari Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amesema wahamiaji zaidi ya 50, wamepewa taarifa kuwa watakuwa miongoni mwa kundi la kwanza litakalosafirishwa hadi nchini Rwanda.../

Tags