May 25, 2022 10:47 UTC
  • Watu zaidi ya elfu 15 wameuawa mashariki mwa DRC tangu mwaka 2007

Raia zaidi ya 15,000 wameuawa kwa sababu ya vita kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita, Wilayani Beni, jimbon Kivu Kaskazini pamoja na Irumu na Mambasa, mkoani Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hii imebainika baada ya kutolewa ripoti ya bunge jijini Kinshasa na wabunge wawili, Tembos Yotama na Mbenzé Mbusa, kulenga maeneo hayo yanayodhibitiwa na waasi wa ADF.

Mauaji hayo yameonekana kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni, ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kati ya mwaka 2008 hadi 2012 ambapo ni chini ya asilimia moja ya raia, 15,500 ndio waliouawa.

Hata hivyo, kati ya mwaka 2013 hadi 2018 hali ilikuwa mbaya zaidi, kufuatia kuuawa kwa raia zaidi ya elfu nane.

Katika ripoti hiyo ya kurasa zaidi ya elfu moja, mwaka 2020 kulikuwa na mashambulizi 989 katika miji kadhaa mashariki mwa DRC na kusababisha watu zaidi ya elfu mbili na mia sita kuuawa, huku wengine zaidi ya elfu nne, wakiuawa mwaka 2021.

Robo tatu ya mauaji hayo yametokea katika kipindi cha miezi 11 baada ya hali ya dharura kutangazwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.../

Tags