Jun 17, 2022 02:17 UTC
  • Kufuta Uingereza safari ya kwanza ya ndege ya kuwahamishia kwa lazima wakimbizi nchini Rwanda

Katika hali ambayo, viongozi wa Uingereza wanang'ang'ania msimamo wao wa kuhamishia nchini Rwanda wakimbizi wanaoomba hifadhi nchini humo, safari ya kwanza ya ndege ambayo ilikusudiwa na Uingereza kuwasafirisha kwa lazima wakimbizi na kuwapeleka nchini Rwanda, imeakhirishwa.

Safari hiyo ya ndege kutoka Uingereza kuelekea Rwanda iliakihirishwa dakika za mwisho siku ya Jumanne, baada ya Bunge la Haki za Binadamu la Ulaya kutoa amri ya kusimamishwa zoezi hilo. Kabla ya hapo na baada ya serikali ya Uingereza kutangaza kuwa kundi la kwanza la wakimbizi waliokimbilia nchini humo lilipangiwa kupelekwa Rwanda siku ya Jumanne, serikali ya Kigali ilisema kuwa, imejiandaa vizuri kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi hao.

Baada ya hukumu hiyo, Priti Patel, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza sambamba na kuashiria kwamba, amekatishwa tamaa na uamuzi huo wa mahakama amesisitiza kuwa, serikali ya Waziri Mkuu Boris Johnson haitalegeza kamba kuhusiana na mpango huo na kwamba, inaanza maandalizi kwa ajili ya ndege nyingine ya kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya Kiafrika ya Rwanda.

Madola ya Ulaya ambayo yanakabiliwa na wimbi la wakimbizi linaloongezeka yameandaa sera maalumu za kukabiliana na hali hiyo.

Viongozi wa Ulaya wamefikia makubaliano ya kutekeleza sera za pamoja kuhusiana na wahajiri na mkakati wa kugawana wahajiri wanaoingia barani humo kupitia Bahari ya Mediterania.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinaweza kuchagua njia moja kati ya njia mbili: Njia ya kwanza ni kuwapokea wahajiri na njia ya pili ni kuyasaidia kifedha mataifa ambayo yanawapokea wakimbizi hao.

Maandamano ya kupinga wakimbizi walioko Uingereza kuhamiishiwa nchini Rwanda

 

Uingereza ni miongoni mwa mataifa ambayo yametangaza hivi karibuni kwamba, itawahamishia nchini Rwanda sehemu ya wakimbizi wanaoomba hifadhi nchini Uingereza na tayari imetiliana saini makubaliano na Rwanda. Kwa mujibu wa mpango wa serikali ya Boris Johnson ni kuwa, watu ambao wanaomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza watahamishiwa nchini Rwanda na kisha mafaili ya maombi yao kujadiliwa huko na kama maombi yao yatakubaliwa basi kwanza watatakiwa waishi nchini Rwanda kwa uchache miaka mitano.

Lakini kama maombi yao yatakataliwa, basi watakuwa na fursa ya kuomba kibali cha kuishi nchini Rwanda ingawa sambamba na hilo, kuna hukumu pia ya kufukuzwa kutoka katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Mpango huo wa Uingereza umekosolewa vikali. Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limeutaja mpango huo kuwa ni fedheha na wa hatari mno na kutangaza kuwa, kutekelezwa kesi ya kwanza ya kuhamishwa wakimbizi, itakuwa sawa na kufunguliwa ukurasa wa giza katika haki za kimataifa za wakimbizi.

Wakimbizi Ulaya Mashariki

 

Wakili anayepinga mpango huo amezungumzia mapungufu katika mfumo wa huduma kwa wakimbizi nchini Rwanda na kutahadharisha kwamba, kuna uwezekano serikali ya Kigali ikawarejesha wakimbizi hao katika nchi zao na hilo linaweza kwenda sambamba na tishio la kiroho, usaili na mateso, hatari ambazo kimsingi ndizo zilizokuwa sababu ya wakimbizi hao kukimbia nchi zao na kuomba hifadhi sehemu nyingine.

Licha ya ukosoaji wote huo, lakini serikali ya Waziri Mkuu Boris Johnson wa Uingereza inang'ang'ania kutekeleza mpango huo ambao umeungwa mkono hata na Mahakama Kuu ya Uingereza. Lakini pamoja na hayo, makundi ya kutetea haki za binadamu yametangaza kuwa, yataendelea na juhudi zao ili kuhakikisha kwamba, mpango huo unafutwa kikamilifu ambapo kufutwa safari ya kwanza ya ndege iliyokuwa ielekee Rwanda ikiwa na wakimbizi inahesabiwa kuwa hatua ya kwanza muhimu ya makundi hayo katika uwanja huo. Hatua hiyo imetajwa na gazeti la The Guardian la Uingereza kwamba, ni pigo kubwa kwa mpango wa serikali na Priti Patel, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza ambaye katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita alipendekeza mpango wa kuwahamishia kwa lazima huko Rwanda wakimbizi wanaoomba hifadhi nchini Uingereza na kufanya kila juhudi kuhakikisha mpango huo unatekelezwa.

Sonya Sceats, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Freedom From Torture anasema: Nimekata tamaa, lakini ninaamini kwamba, mapambano hayajafikia ukingoni na tutatumia kila wenzo kwa ajili ya kuhitimisha mwenendo huu.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Waziri Mkuu wa Uingereza alikuwa ameonya kwamba, nchi yake itajitoa katika Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya.

Priti Patel, Waziri wa Mambo ya ndani wa Uingereza

 

Ukweli wa mambo ni kuwa, serikali ya Uingereza inakusudia kuwapeleka wakimbizi hao mahali ambapo pana umabli wa kilomita 6,000 kutoka Uingereza ikiwa na lengo la kuiga sera za Australia katika uwanja huo. Kuwahamishia wakimbizi nje ya nchi fulani ni sehemu ya mpango mkubwa zaidi wa kimkakati ambao unatekelezwa na baadhi ya mataifa ikiwemo Australia. Mataifa hayo yanawahamishia wakimbizi katika nchi zenye kipato kidogo na masikini iolii kwa njia hiyo ziepukane na matatizo ya wakimbizi hao. Hatan hivyo mataiifa tajiri kama Uingereza na Australia yamekuwa yakitoa ahadi kubwa ya fedha kwa nchi masikini ambazo zitakuwa tayari kuwapokea wakimbizi na wahajiri hao. Kwa mfano, pendekezo la awali la Uiingereza kwa TRwanda ni kuipatia pauni milioni 120.

Filihali licha ya kufutwa safari ya kwanza ya ndege iliyokuwa iwapeleke wakimbizi nchini Rwanda kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya, lakini mpango huop wa Uingereza bado ungali;po na viongozi wa taifa huiilo la Ulaya wametangaza kuwa, watautekeleza tu mpango huo. Kwa utaratiibu huo inaonekana kuwa, wakimbizi watakabiliwa na kipindi kigumu zaidi katika sikuu za usoni pamoja na kuweko nara nyingi zinatolewa na Uingereza kuhusiana na suala zima la haki za binadamu. 

Tags