Jul 01, 2022 10:53 UTC
  • Balozi wa Iran nchini Kenya: Bidhaa za ujenzi za Iran kuuzwa Afrika

Balozi wa Iran nchini Kenya amesema: Bidhaa za ujenzi vya Iran hasa marumaru kutoka mkoani Yazd katikati mwa Iran zitasafirishwa kwenda kwenye masoko ya nchi za Kiafrika ikiwemo Kenya.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, "Jafar Barmaki", balozi wa Iran nchini Kenya, wakati wa safari yake katika mkoa wa Yazd akiwa na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Kenya, alihudhuria maonyesho ya kudumu ya marumaru katika eneo la Meybod, ili kujadili njia za kuamsha uchumi wa eneo hilo.

Akizungumzia  na maafisa wa eneo hilo kuhusu uwezo wa soko la nchi za Afrika Mashariki hususan Kenya, balozi wa Iran amesema: "Maonyesho ya kudumu ya bidhaa na vifaa vya ujenzi vya Iran yataanzishwa nchini Kenya hivi karibuni.”

Barmaki ameeleza matumaini yake kuwa hivi karibuni bidhaa za Iran, hasa katika uwanja wa marumaru, ambavyo vina kiwango cha juu na kwa bei nafuu, vitauzwa nje ya nchi kwenye soko la Kenya na nchi za Afrika Mashariki ambazo zina uwezo mzuri katika nyanja ya ujenzi.

Akizungumzia kasi kubwa ya ujenzi na ukuaji wa asilimia 12 katika sekta ya ujenzi nchini Kenya, balozi wa Iran nchini Kenya ameongeza: “Sera ya serikali ya Kenya ni kuzalisha kwa wingi na kuzalisha nyumba za bei nafuu, na hii ni fursa nzuri kwa wazalishaji wa Iran nchini humo.”