Jul 06, 2022 07:39 UTC
  • Moncef Marzouki
    Moncef Marzouki

Rais wa zamani wa Tunisia, Moncef Marzouki, amekosoa rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo ambayo ilizinduliwa na Rais Kais Saeid wa nchi hiyo.

Kais Saeid, Rais wa Jamhuri ya Tunisia, hivi karibuni alizindua rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo ambayo imezidisha madaraka ya Rais.

Moncef Marzouki, rais wa zamani wa Tunisia amesema kuwa rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo iliyozinduliwa na Kais Saeid ni matokeo ya unjozi za mtu mmoja na hata walioshiriki katika uandishi wake wameipinga na kuipiga vita.

Awali Marzouki aliwataka Watunisia wapuuze rasimu hiyo iliyozinduliwa na Kais Saeid na badala yake wasusie kura hiyo ya maoni ya rasimu kupitia propaganda za kitaifa zitakazoshirikisha vyama na makundi yote vya kisiasa na kiraia.

Rais wa zamani wa Tunisia pia ameonya kuhusu kujirudia hali ya Sudan nchini Tunisia na kuchukua madaraka utawala wa kijeshi.

Siku chache zilizopiita pia Mkuu wa Kamati ya Katiba ya Tunisia alitangaza upinzani wake dhidi ya rasimu ya katiba mpya iliyotangazwa na Rais Kais Saeid wa nchi hiyo, akisema kuwa kiongozi huyo anapigania kuwepo katiba ya upande mmoja.

Sadok Belaid ambaye ni profesa wa zamani katika masuala ya sheria na katiba amesema kuwa, rasimu iliyozinduliwa na Rais wa Tunisia ni hatari na haiendi sambamba na rasimu ya awali iliyotayarishwa na kamati hiyo. 

Sadok Belaid

Tunisia inatarajia kuitisha kura ya maoni kuhusu katiba mpya tarehe 25 mwezi huu wa Julai. Kwa mujibu wa rasimu iliyopendekezwa na Rais Saeid kwa ajili ya katiba mpya, Rais Saeid ataruhusiwa kuwasilisha miswada ya sheria na kuwa na mamlaka makubwa ya kupendekeza mikataba mbalimbali na kuandaa bajeti za serikali.  

Katika siku za karibuni, Watunisia wamemimika katika mitaa na barabara za nchi hiyo wakipinga rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Rais wao. 

Tags