Jul 07, 2022 03:37 UTC
  • Jeshi la Algeria lafanya maneva kubwa zaidi katika miongo mitatu ya karibuni

Jeshi la Algeria limefanya maneva makubwa zaidi kuwahi kutekelezwa nchini humo katika kipindi cha miaka 33 ya karibuni katika kuadhimisha siku ya uhuru wa nchi hiyo.

Algeria ilipata uhuru Julai 5 mwaka 1962; baada ya miaka saba ya vita na mapabano ya kupigania ukombozi wa nchi hiyo kutoka kwa mkoloni Ufaransa. Uhuru wa Algeria unahesabiwa kuwa mapinduzi makubwa yaliyojiri katika karne ya ishirini.  

Shirika la habari la Russia al Yaum limeripoti kuwa, Algeria jana Jumatano iliadhimisha kutimia mwaka wa sitini  tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka kwa mkoloni Ufaransa mwaka 1962; katika sherehe zilizohudhuriwa pia na Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika mji mkuu wa nchi hiyo, Algiers. 

Ismail Hania ashiriki katika maadhimisho ya uhuru wa Algeria 

Nukta muhimu katika maneva hayo ya jeshi la Algeria ni kushuhudia uwepo wa Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama ya Palestina (Hamas) pamoja na viongozi wengine wa nchi mbalimbali duniani.  

Algeria ni moja ya nchi waungaji mkono wakuu wa wananchi wa Palestina katika miongo kadhaa ya karibuni katika eneo la Asia Magharibi na kaskazini mwa Afrika. Nchi hiyo imeendelea kuwaunga mkono wananchi wa Palestina licha ya baaadhi ya nchi jirani zake kuchukua hatua ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni. Algeria imedhihirisha wazi wazi upinzani wake kwa hatua yoyote ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Israel.