Jul 19, 2022 08:07 UTC
  • Taasisi nchini Tunisia zataka kufutwa kura ya maoni kuhusu katiba

Taasisi 40 na wananchi wa Tunisia wamemtaka Rais wa nchi hiyo Kais Saeid kuacha kuendesha kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.

Kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya ya Tunisia ilipangwa kufanyika tarehe 27 mwezi huu. Baada ya kuchapishwa nakala ya kwanza ya rasimu ya katiba mpya ya Tunisia mnamo Juni 30, nakala iliyofanyiwa marekebisho ya rasimu hiyo tajwa ilichapishwa katika gazeti la serikali tarehe 9 mwezi huu wa Julai. 

Leo Jumanne taasisi 40 na wananchi wa Tunisia wamewasilisha taarifa yao kwa Rais Kais Saeid wa Tunisia ikieleza kuwa: "tunamtaka rais kusikia sauti za wananchi na mirengo ya kiraia inayoshinikiza kuhusu utawala wa kidemokrasia." 

Rais Kais Saeid wa Tunisia 

Jumuiya na mirengo hiyo ya wananchi wa Tunisia aidha imetilia mkazo kuheshimiwa na kutiliwa maanani masuala ya kitaifa, haki yao ya kuwa huru, utu na usawa na njia ya mapinduzi.  

Wakati huo huo, Rashid Ghanoush Mkuu wa Chama cha Kiislamu cha An Nahdhah cha Tunisia Ijumaa iliyopita alieleza kuwa Rais Kais Saeid wa nchi hiyo anatumia kura ya maoni ya katiba mpya ili kuurejesha nchini utawala wa kidikteta. Amesema anga iliyojitokeza sasa huko Tunisia kabla ya kufanyika kura hiyo ya maoni si ya kidemokrasia.

Tags