Jul 19, 2022 12:31 UTC
  • Wakenya waipongeza serikali kwa kupunguza bei ya unga wa ugali

Wakenya wamefurahia hatua ya serikali kupunguza bei ya unga wa mahindi. Baadhi ya Wakenya wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kushukuru hatua ya serikali kupunguza bei ya unga wa mahindi.

Serikali ya Kenya imepunguza bei ya pakiti ya unga wa kilo 2 kutoka shilingi 200 hadi shilingi 100. Baada ya hatua hiyo ya serikali ya Uhuru Kenyatta, wananchi wameitaka serikali kuzingatia kutoa ruzuku kwa bei ya bidhaa nyingine muhimu kama vile mafuta ya kukaangia.

Mafuta ya kukaangia katika maduka makubwa kote nchini yanauzwa kwa kati ya shilingi 450 na 740 kwa lita.

Bei ya Unga katika maduka makubwa iliongezeka baada ya wasagaji kuonya kuhusu uhaba wa mahindi nchini Kenya.

Hatua hiyo ya serikali imewapa ahueni Wakenya wengi waliokuwa tayari wanaanza kulemewa na gharama ya juu ya maisha.

Serikali Kenya yapunguza bei ya unga wa ugali

Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) iliripoti mnamo Juni 2022 kwamba bei za bidhaa za msingi za kutumia nyumbani ziliongezeka kwa asilimia 13.8 na kupanda kwa mfumuko wa bei hadi asilimia 7.9. Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wamepongeza hatua hiyo, na kuitaka serikali kuzingatia bei ya bidhaa nyingine muhimu kama vile mafuta ya kupikia.

Lita moja ya mafuta ya kupikia katika maduka makubwa kote nchini Kenya inauzwa kwa shilingi 450 mpaka 740.

Tags