Jul 22, 2022 02:36 UTC
  • Amnesty yaitaka serikali ya Ethiopia ifanye uchunguzi kuhusu mauaji ya raia zaidi ya 400

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeitaka serikali ya Ethiopia iendeshe uchuguzi kuhusiana na mauaji ya kikabila ya raia zaidi 400 yaliyofanyika katika eneo la Oromia.

Amnesty International limeyataja mauaji hayo kuwa ya kutisha, kutokana na kwamba mauaji mengine yalifanyika pia katika wilaya tofauti ya eneo hilo.

Vurugu hizo zilizoshuhu diwa katika wilaya za Tole na Gimbi zilielekezwa dhidi ya raia wakulima wa eneo la Amhara.

Kundi la watu wenye silaha la Oromo Liberation Army (OLA), linatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo, huku serikali ya Addis Ababa ikikosolewa kwa kutochukua hatua ya kukabiliana na wahusika wa mauaji hayo.

Mashuhuda wanasema vikosi vya serikali viliwasili kwa kuchelewa eneo la tukio na muda mrefu baada ya washambuliaji hao kuondoka.

Hata hivyo kundi la OLA, limekanusha kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea eneo la Oromia likilituhumu kundi ambalo linadai linafadhiliwa na serikali.

Serikali ya Ethiopia ilikuwa imeahidi kuendesha uchuguzi na kuwachukulia hatua wahusika, lakini raia wengi eneo hilo wana shaka na uchunguzi huo unaodaiwa kufanywa na serikali.../

Tags