Aug 06, 2022 07:35 UTC
  • Algeria na Tunisia zalaani kuuliwa wananchi madhulumu wa Palestina

Wizara za Mambo ya Nje za Algeria na Tunisia zimelaani hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwaua wananchi madhulumu wa Palestina.

Utawala wa Kizayuni jana Ijumaa ulitekeleza mashambulizi ya anga katika maeneo kadhaa ya Ukanda wa Ghaza na kuwaua shahidi Wapalestina 10 akiwemo mtoto wa miaka 5 na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina. Wapalestina wengine 80 wamejeruhiwa. 

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria leo asubuhi imetoa taarifa ikilaani mauaji ya wananchi madhulumu wa Palestina yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel na kueleza kuwa, mauaji hayo yameongeza mlolongo wa hatua za ukiukaji wa sheria za kimataifa zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina. 

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imesisitiza udharura wa kushikamana kikamilifu nchi hiyo na wananchi wa Palestina. Algeria aidha imeitolea wito jamii ya kimataifa hususan Umoja wa Mataifa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ili kusitisha mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa Palestina, kuheshimu haki za wawanchi wa Palestina na kuwezesha wananchi hao kupata haki yao ya kunda nchi huru ya Palestina, mji mku wake ukiwa Quds Tukufu. 

Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imelaani hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza na kuitaka jamii ya kimataifa kutekeleza majukumu yake mkabala wa Palestina. Utawala haramu wa Israel umeliwekea mzingiro wa nchi kavu, baharini na anga eneo la  Ukanda wa Ghaza  tokea mwaka 2006; huku wakazi wa eneo hilo wakitaabika na matatizo chungu nzima yakiwemo ya matibabu n.k.

Raia wa Ukanda wa Ghaza chini ya mzingiro wa kiuchumi wa Israel 

 

Tags