Aug 08, 2022 11:44 UTC

Waislamu wa madhehebu ya Shia mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, wameshiriki katika hafla ya maombolezo ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussain (AS) katika siku ya Ashura.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iranpress, mamia ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wameshiriki katika kikao cha maombolezo katika Msikiti wa Park Road katika mji mkuu wa Nairobi, ambapo Hujjatul Islam wa al-Muslimin Muhammad Mwega alitoa hotuba kuhusu umuhimu wa mwamko wa Karbala.

 Waombolezaji wa Imam Hussein jijini Nairobi  kisha walishiriki katika matembezi ya Siku ya Ashura na wakasoma mashairi kuhusu Imam Husein AS na masahaba zake.

Waumini katika Msikiti wa Park Road Nairobi katika maombolezo ya Siku ya Ashura

 

Taarifa zinasema Waislamu katika maeneo mengine ya Kenya kama vile Mombasa, Nakuru na Kisumu pia wameshiriki katika vikao vya kukumbuka Masaibu ya Imam Hussein AS katika Siku ya Ashura.

Maombolezo ya Ashura pia yamefanyika katika nchi zingine za Afrika kama vile Tanzania, Uganda, Ghana na Nigeria.