Aug 14, 2022 02:30 UTC
  • Tunisia: Wahamiaji 82 wamekamatwa au kuokolewa wakijaribu kuelekea Ulaya

Mamlaka za Tunisia zimesema kuwa, zimezuia majaribio matano mapya ya uhamiaji haramu wa usiku kucha na kuwaokoa au kuwakamata watu 82.

Vitengo vya Walinzi wa Taifa kutoka kaskazini, katikati, kusini na pwani ya Tunisia vilizuia majaribio "kama sehemu ya vita dhidi ya uhamiaji usio wa kawaida", ilisema taarifa.

Tunisia ni nchi jirani na Libya na ni sehemu muhimu ya kuondokea wahamiaji wenye ndoto za kufika Ulaya na sana nchini Italia. Kunafanyika majaribio mengi ya kuvuka bahari ya  Mediterranean hasa wakati wa majira ya joto.

Taarifa zinasema kuwa, watu 76 waliokolewa katika operesheni nne za baharini, na wengine sita walikamatwa nchi kavu katika maeneo ya Gabes na Sfax huko Uhispiania usiku wa kuamkia jana Jumamosi.

Hata hiyo taarifa hiyo haikusema wahajiri hao ni raia wa nchi gani na wala haikutoa maelezo kuhusu aina ya boti walizokuwa wanatumia. 

Wahamiaji wengi haramu huishia kufa maji kwa tamaa ya kuelekea Ulaya na ndoto zao za alinacha

 

Taarifa hiyo pia imesema kuwa, wahajiri hao wamekamatwa na fedha za kigeni na fedha za Tunisia ingawa pia haikusema ni kiasi gani cha fedha hizo. 

Vyombo vya habari katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini viliripoti ajali ya meli siku ya Jumanne iliyotokea kwenye visiwa vya Kerkennah ambapo watu wananewalifariki dunia na wote walikuwa ni raia wa Tunisia - wanawake watatu, watoto wanne na mwanamume mmoja. Watu wengine 20 waliokolewa.

Siku ya Jumapili pia, maafisa wa Gadi ya Ufukweni ya Tunisia walisema kuwa watu 170 kutoka nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara walikuwa miongoni mwa wahamiaji 255 waliokamatwa wakati wa majaribio 17 ya kuvuka bahari kuelekea Ulaya.