Sep 07, 2022 08:02 UTC
  • Uganda yapiga marufuku tamasha la muziki 'lisilo la maadili' linalohusishwa na ngono na dawa za kulevya

Uganda jana ilipiga marufuku tamasha la muziki la kielektroniki lisilo la maadili ambalo linaathiri maadili na tabia za watoto katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Tamasha hilo ambalo huko nyuma liliwakusanya watu wasiopungua elfu kumi wakiwemo watalii kutoka nje ya nchi lilitazamiwa kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia Septemba 15 katika mji wa Jinja kusini mashariki mwa Uganda. 

Hata hivyo siku kadhaa kabla ya kufanyika tamasha hilo la muziki wa kielektroniki lililo kinyume na maadili ambalo lilisimama kwa miaka kadhaa kutokana na  na janga hatari la Corona; bunge la Uganda lilitangaza katika akaunti yake ya mtandao wa twitter kwamba limepiga marufuku tamasha hilo kwa jina la "Nyege Nyege Festival."

Kupigwa marufuku tamasha haribifu la muziki Uganda 

Rose Lilly Akello Waziri wa Maadili na Uadilifu wa Uganda amesema kuwa tamasha hilo linachochea mporomoko wa maadili ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya na vitendo vya uasherati na akasema hawataki kuona ukosefu huu wa maadili ukiiathiri Uganda. 

Naye Martin Mugarura Waziri wa Utalii wa Uganda amesema kuwa kupigwa marufuku kwa tamasha hilo la muziki kutakuwa na athari hasi kwa uchumi wa Uganda ambao unajikongoja kuinukia kutokana na janga la Corona.  

Neno "Nyege Nyege" linamaanisha hamu isiyozuilika ya kucheza ngoma katika lugha ya Kiganda lakini pia inaweza kuwa na maana ya ngono katika lugha nyingine za nchi hiyo na Afrika kwa ujumla. Tayari zaidi ya watalii 8000 walikuwa wamenunua tiketi kwa ajili ya kushuhudia tamasha hilo haribifu la muziki; ambapo watalii hao walitarajia kusalia nchini humo katika kipindi chote cha tamasha hilo tajwa na hata baada ya kumalizika. Uhusiano wa  watu wa jinsia moja umeenea nchini Uganda; ambapo mwezi Disemba mwaka 2013 nchi hiyo ilipitisha sheria inayoadhibu vitendo vya ushoga.  

 

 

Tags