Sep 14, 2022 12:05 UTC
  • Watu 10 wauawa katika mashambulio kwenye jimbo la Tigray, Ethiopia

Taarifa kutoka kaskazini mwa Ethiopia zinasema kuwa, waasi wasiopungua 10 wa TPLF wanaopigania kujitenga jimbo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia wameuawa sambamba na kuanza mapigano mapya kati ya wanajeshi wa serikali na waasi hao.

Mapigano baina ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray yalianza mwezi Novemba 2020 na mbali na kusababisha ukosefu mkubwa wa usalama, yamepelekea watu wengi kuuawa na kujeruhiwa na mamilioni ya wakazi wa jimbo hilo kuishi katika mazingira magumu sana. Mashirika ya kimataifa yanasema kuwa, wakazi hao wa kaskazini mwa Ethiopia hivi sasa hawana hata maji salama ya kunywa, hawana chakula na mahitaji yao ya kimsingi kabisa. 

Zaidi ya hayo, Ethiopia imekumbwa na machafuko ya kikabila katika maeneo mengi ambayo mengi yake yanatokana na malalamiko ya muda mrefu na ugomvi wa kihistoria wa kisiasa.

Shirika la habari la IRNA limetangaza leo Jumatano kuwa, wanajeshi wa Ethiopia wamefanya mashambulizi mawili pacha ya droni huko Tigray, huku duru za hospitali zikithibitisha kuuawa watu wasiopungua kumi katika mashambulio hayo.

 

Jana usiku msemaji wa waasi wa TPLF alisema kuwa, jeshi la Ethiopia limetumia ndege zisizo na rubani na kuua na kujeruhi watu wengi katika mji wa Makele ambao ndiyo makao makuu ya jimbo la Tigray.

Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray TPLF waliokuwa ndio watawala wa muda mrefu nchini Ethiopia kwa zaidi ya miaka 30 wamekuwa wakilidhibiti wao jimbo la Tigray.

Watu naokadiriwa milioni 2.5 wamekuwa wakimbizi katika maeneo ya kaskazini mwa Ethiopia tangu vilipoanza vita mwaka mmoja uliopita.

Tags