Sep 18, 2022 08:12 UTC
  • Kiongozi wa Ennahdha kusailiwa na polisi ya Tunisia madai ya 'ugaidi'

Kiongozi wa chama cha Kiislamu chenye ushawishi mkubwa nchini Tunisia cha Ennahdha anatazamiwa kusailiwa na jeshi la polisi la nchi hiyo kesho Jumatatu.

Maafisa wa chama hicho wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, Rached Gannouchi na afisa mwingine mwandamizi wa chama hicho, Ali Larayedh wameitwa na polisi ili kusailiwa juu ya uchunguzi unaoendelea kuhusu mitandao ya kuwapeleka watu nchini Syria kwa ajili ya kupigana.

Harakati ya Ennahda inakanusha madai ya kuwa na uhusiano wa aina yoyote na faili hilo, na inasema kwamba hiyo ni kampeni inayolenga kuchafua jina la chama hicho kikubwa zaidi cha upinzani nchini Tunisia. 

Chama cha Ennahdda nchini Tunisia kimelaani vikali kile kilichoeleza kuwa ni kukamatwa kiholela kwa watu kadhaa akiwemo kiongozi wa ngazi ya juu wa harakati hiyo, Habib Al-Louz na kutaka waachiliwe huru mara moja.

Harakati hiyo imetaka kukomeshwa kwa kampeni ya kukamata watu, huku ikilaani kampeni za vyombo vya habari zenye nia mbaya zilizoanzishwa na baadhi ya pande zinazojulikana kuwa na chuki dhidi ya chama hicho cha Kiislamu.

Rais Saeid

Hatua za rais Kais Saied za kunyakua madaraka ya nchi zilizofikia kilele kwa katiba mpya iliyopitishwa kwa kura ya maoni mnamo mwezi Julai, na ambayo ilisusiwa na akthari ya Watunisia.

Wapinzani wanasema hatua hiyo ni sawa na kurejea kwenye utawala wa kiimla, katika nchi pekee yenye demokrasia iliyotokana na vuguvugu la Machipuo ya Kiarabu ya mwaka 2011.

Tags