Sep 18, 2022 08:16 UTC
  • Maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein yafanyika Tanzania, Nigeria, Niger

Waislamu ya madhehebu ya Shia Tanzania, visiwani Zanzibar, Nigeria na Niger wamefanya marasimu, matembezi na vikao vya kuadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (AS).

Huko nchini Nigeria, mamia ya watu walishiriki katika matembezi hayo ya Arubaini ya Imam Hussein (AS) jana Jumamosi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Baadaye walikusanyika katika Husseiniya ya Baqiyatullah katika mji wa Zaria. Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky aliuhutubia mkusanyiko wa waombolezaji hao na kusema, matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS yataendeleaa hadi atakapodhihiri Imam Mahdi AS.

Amesema Waislamu wa Nigeria wamefanya matembezi hayo kwa njia ya amani katika vituo kadhaa katika miji na majimbo ya Kano, Kastina, Zamfara, Sokoto, Kaduna, Bauchi na Plateau.

Arubaini Nigeria

Jeshi la polisi la Nigeria huko nyuma limekuwa likiwashambulia Waislamu wanaoshiriki katika matembezi ya Arubaini ya Imam Husain AS na kuua shahidi kadhaa miongoni mwao.

Vikao na matembezi ya tukio la kila mwaka ambalo linaadhimisha siku ya 40 baada ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), Imam wa tatu wa madhehebu ya Shia yamefanyika nchini Niger.

Tags