Sep 25, 2022 02:43 UTC
  • Ripoti: Zaidi ya watu milioni 37 wanataabika na njaa Pembe ya Afrika

Inaelezwa kuwa, zaidi ya watu milioni 37 katika eneo la Pembe ya Afrika wanataabika na baa la njaa ambayo imechangiwa na ukame mbaya sana, ambao umeua takriban wanyama milioni 9.

Hayo yamo katika ripoti ya mashirika ya misaada ya kibinadamu ambayo yametahadharisha kwamba, hali ni mbaya sana na kuna uuwezekanao wa kutokea maafa ya kibinadamu.

Wajuzi wa mambo wanasema kuwa, ikichangiwa na matokeo ya janga la Covid-19 na vita vya Russia nchini Ukraine, hali ya njaa ulimwenguni inazidi kuwa mbaya zaidi siku hadi siku.

Mashirika mbalimbali ya misaada ya kibinadamu yamekuwa yakitoa ripoti mara kwa mara na kuutahadharisha kuhusiana na hali mbaya ya ukosefu wa chakula hususan katika eneo la Pembe ya Afrika na Sahel Afrika.

 

Hivi karibuni zaidi ya asasi 200 za kiraia zilitoa mwito wa kuchukuliwa hatua kwa ajiili ya kukabiliana na janga la njaa ulimwenguni ambalo linazidi kuongezeka siku baada ya siku.

Ripoti zinaeleza kuwa, watu wapatao milioni 345 wanataabika na baa la njaa katika maeneo mbalimbali ya dunia, idadi ambayo ni maradufu ikilinganishwa na mwaka 2019.

Hata hivyom maeneo yanayokabiliwa zaidi na hatari ya baa la njaa ni Pembe ya Afrika, Sahel Afrika, Afghanistan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan na Yemen.

Tags