Oct 03, 2022 10:09 UTC
  • Miripuko ya kigaidi yaua watu watano nchini Somalia

Miripuko miwili ya kigaidi imetokea leo Jumatatu huko Somalia na kuua watu watano na kujeruhi watu wengine kadhaa.

Gavana wa jimbo la Hairan huko Somalia amesema kwamba miripuko hiyo iliyotokea katika kituo cha kijeshi katika eneo la Baladwain la katikati mwa Somalia imepelekea watu kadhaa waliokuwa katika eneo la tukio kujeruhiwa, baadhi wakiwa katika hali mahututi.

Kundi la kigaidi la as-Shabaab ambalo lina mfungamano wa karibu na kundi jingine la kigaidi la al-Qaida limetangaza kuhusika na na miripuko hiyo.

Kundi la kigaidi la as-Shabaab limekuwa likijaribu kuipindua serikali kuu ya Somalia tangu mwaka 2007.

As-Shabaab walifukuzwa Mogadishu na Jeshi la Somalia na vikosi vya Umoja wa Afrika mwaka 2011, hata hivyo, kundi hilo la kigaidi bado linadhibiti maeneo makubwa ya vijijini nchini humo.