Uchambuzi
-
Kujaribiwa irada na nguvu ya Iran; kosa la kistratijia la Netanyahu
Apr 16, 2021 08:02Kumetokea mvutano kati ya utawala haramu wa Israel na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufuatia hatua ya utawala huo ya kufanya uharibifu katika kutuo cha urutubishaji urani cha Iran katika eneo la Natanz, uharibifu ambao umetajwa na Iran kuwa ni ugaidi wa kinyuklia.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu kuhusu mazungumzo ya nyuklia; sharti la Iran, msingi wa kuhuishwa JCPOA
Apr 16, 2021 03:35Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, siasa za Iran kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ziko wazi, na maafisa wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya kuhuishwa makubaliano hayo wanapaswa kuwa macho ili yasirefushwe kupita kiasi, suala ambalo lina madhara kwa taifa.
-
Mauzo ya silaha ya serikali ya Biden kwa Imarati
Apr 15, 2021 08:15Miezi kadhaa ikiwa imepita tokea Joe Biden atangaze kusimamisha na kutazmwa upya mkataba wa mauzo ya silaha za Marekani kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), rais huyo mpya wa Marekani ametangaza kuwa ataendelea na mpango wa awali wa kuiuzia nchi hiyo ya Kiarabu silaha zenye thamani ya dola bilioni 23, ikiwa ni pamoja na ndege za kivita aina ya F35, droni zenye kubeba silaha na zana nyinginezo za kivita
-
Kimya cha IAEA baada ya uharibifu uliofanywa katika taasisi ya nyuklia ya Iran
Apr 15, 2021 02:25Hujuma ya uharibifu iliyofanywa na Israel katika taasisi ya nishati ya nyuklia ya Natanz nchini Iran siku ya Jumapili iliyopita, kwa mara nyingine tena imeleta udharura wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kama taasisi kuu zaidi ya kimataifa inayosimamia shughuli za nyuklia dunia, kutoa jibu na kueleza wazi msimamo wake.
-
Vikwazo vipya vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Iran; kwenda sambamba na Washington na Tel Aviv
Apr 14, 2021 12:48Baraza la Umoja wa Ulaya Jumatatu tarehe 12 mwezi huu wa Aprili liliwajumuisha maafisa 8 na taasisi 3 katika ordha ya vikwazo dhidi ya Iran kwa kisingizio cha eti kukiuka haki za binadamu. Aidha baraza hilo limechukua uamuzi wa kurefusha hatua zake dhidi ya Iran hadi tarehe 13 mwezi Aprili mwaka kesho kwa kisingizio cha kile ilichokitaja kuwa ukiukaji wa haki za binzdamu.
-
Kukiri Biden juu ya kuudhiwa na kubughudhiwa Waislamu nchini Marekani
Apr 14, 2021 02:22Rais Joe Biden wa Marekani amekiri katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuwadia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani juu ya kuudhiwa na kubughudhiwa Waislamu katika jamii ya Marekani.
-
Safari ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia mjini Tehran; sisitizo la azma ya pamoja ya kupanua ushirikiano wa kistratejia
Apr 13, 2021 10:45Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia Jumannae ya leo Aprili 13 amekutana na kufanya mazungumzo hapa mjini Tehran na Dakta Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo wawili hao wamejadili na kuzungumzia masuala muhimu ya pande mbili, kieneo na kimataifa.
-
Waungaji mkono wa nje wa Hariri ndio chanzo cha kushindwa kwake kuunda serikali ya Lebanon
Apr 13, 2021 02:52Licha ya kupita miezi 6 tokea bunge la Lebanon limpigie kura ya kuwa na imani naye, Saad Hariri ameshindwa kuunda serikali mpya na kwa sasa masuala ya nchi hiyo yanasimamiwa na serikali ya muda inayoongozwa na Hassan Diab.
-
Tukio la Natanz; udharura wa jamii ya kimataifa na IAEA kukabiliana na ugaidi wa kinyuklia
Apr 12, 2021 11:25Jumapili alfajiri kulijiri tukio la kigaidi katika mfumo wa usambazaji umeme wa kituo cha urutubishaji urani cha Natanz hapa nchini.
-
Viongozi wa Msumbiji waeleza wasiwasi wao kuhusiana na harakati za kundi la Daesh nchini humo
Apr 12, 2021 02:51Katika miaka ya hivi karibuni makundi ya kigaidi yameimarisha harakati zao katika nchi mbalimbali za Kiafrika. Genge la Daesh ni miongoni wa makundi hayo ya kigaidi ambayo yamezidisha mashambulizi na harakati zao katika nchi za Afrika.